Top Stories

“Nani kasema sigombei Mwaka 2025?, wameanza kutuchokoza”- Rais Samia

on

NI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambapo leo ameshiirki katika  maadhimisho ya siku ya Demokrasia duniani.

Shughuli hii inafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam.

Na katika kuhitimisha hotuba yake Rais Samia Suluhu Hassan alizungumzia sakata lililoendelea mitandaoni kwa wanaosema kuwa hatogombea urais 2025.

“Leo hii Wanawake mmempa Tuzo Rais wenu, Rais Mwanamke kwa bashasha na furaha kubwa lakini nataka niwaambie Wanawake bado hatujaweka Rais Mwanamke, tulichokichangia sisi ni ile kusukuma mpaka Mwanamke akawa Makamu wa Rais, lakini kufika hapa kama isingekuwa kudra ya Mungu ingekuwa ngumu sana”

“Sasa Ndugu zangu Rais Mwanamke tutamuweka Mwaka 2025, Wanawake Oyeee, Tanzania Oyee, Ndugu zangu Mwaka 2025 tukifanya vitu vyetu vizuri, tukishikamana, tukimuweka Rais wetu tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana, wameanza kutuchokoza, kuandika kwenye vigazeti ‘Samia hatosimama (kugombea Urais)’ nani kawaambia!?”- Rais Samia

Ayo TV & Millardayo.com imekuwekea video hii ufahamu kile alichozungumza Rais Samia Suluhu Hassan.

KWA MARA YA KWANZA KIKWETE KAFUNGUKA UTENDAJI KAZI WA RAIS SAMIA “MPAKA SASA ANAENDESHA NCHI VIZURI”

 

Soma na hizi

Tupia Comments