social network

Unachotakiwa kujua kutoka kwa Nape Nnauye kuhusu CCM

on

Usiku wa April 25 2017 Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi kupitia tiketi ya CCM Nape Moses Nnauye ametumia ukurasa wake wa twitter kuandika ujumbe wake wa wazi aliyowahi kuandika kipindi cha nyuma kuhusu CCM, lengo likiwa ni kuweka kumbukumbu sawa kwa watu kuhusu CCM.

Nape ametumia ukurasa wake wa twitter kupost screen shot za tweet zake za zamani na kuandika neno KUWEKA KUMBUKUMBU SAWA “Watu wengi wanaamini nimeisaidia sana CCM lakini ukweli ni kuwa CCM imenisaidia sana mimi kuliko mimi nilivyoisaidia, CCM ni SHULE” >>> Nape

Screenshot ya pili ya Nape Nnauye ambapo zote zinaonesha ni tweet ambazo aliziandika December 15 2016 ila usiku wa leo ameamua kuzikumbushia akisema ni kuweka kumbukumbu sawa “Bahati niliyopata kwa kuwa muenezi CCM ni kufanya kazi na ndg Kinana ni mwema, mzalendo, hodari, uwezo mkubwa, upendo na maarifa mengi” >>> Nape

VIDEO: Maswali mawili ya Nape Nnauye bungeni April 24 2017

Soma na hizi

Tupia Comments