Mbunge wa Mtama ambaye pia alishawahi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye alikubali kukaa kwenye exclusive interview na Ayo TV namillardayo.com kuzijibu na kuzitolea ufafanuzi tuhuma za kuikosoa serikali baada ya kuondolewa kwenye nafasi ya Uwaziri.
“Kwanza ni vizuri watu wakaelewa kwamba Wabunge kutoa mawazo na kushauri hakuna maana ya kuikosoa serikali au kumdhalilisha Rais na serikali yake bali ni wajibu wetu kama wabunge.
“Sisi kama wabunge tuna hasa wa CCM ndio zaidi tunapaswa kuishauri vizuri serikali ili utekelezaji wa Ilani utekelezeke.
“Kuna watu wanahoji kwanini sasa hivi naonekana kuishauri serikali sasa hivi nikiwa mbunge wa kawaida, Unajua ukiwa Waziri na wewe unakuwa ni sehemu ya serikali na mnashauriana katika vikao vya ndani.
“Wanaosema kwanini sasa hawajui nilikuwa nafanya nini nikiwa ndani ya serikali na hayo ni mawazo yao, Ukiwa mbunge nafasi yako ni ndani ya bunge hivyo naitumia nafasi yangu vizuri kwa mujibu wa katiba nikiwa kama Mbunge.” – Nape Nnauye
VIDEO: ‘Ukombozi wowote una vita, vita hii isituumize’ –Nape