Club ya Napoli ya Italia imeshindwa kisheria na watoto wa legend wa club hiyo Diego Maradona kuhusiana na kutumia picha (image) ya Maradona katika jezi zao.
Baada ya Maradona kufariki Dunia 25 November 2020, club ya Napoli iliamua kumuenzi legend huyo kwa kutengeneza jezi zenye sura ya Maradona kama sehemu ya kumuenzi staa huyo aliyewahi kuichezea club hiyo kwa miaka 7 (1984-1991).
Sasa Napoli wameshindwa kesi ya kisheria na watoto watano wa Maradona hivyo kuanzia sasa Napoli hawaruhusiwi kutumia picha ya Maradona popote.
Napoli walisema kuwa haki ya kutumia picha na alama za vidole (fingerprint) za Maradona katika jezi walipewa na meneja wa legend huyo Ceci ila sasa familia imeshinda kesi na sasa wametakiwa kusitisha mara moja.