Michezo

Du!! Samir Nasri ana msimamo huu kuhusu timu yake ya taifa hata kama baba yake angekuwa kocha…

on

Wachezaji wengi wa soka duniani hupenda kuona wakiitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi zao hususani katika michuano mikubwa kama Kombe la Dunia na michuano mingine ambayo itawapa fursa na heshima sehemu mbalimbali. Kiungo wa kimataifa wa Kifaransa ambaye anaitumikia klabu ya Manchester City ya Uingereza Samir Nasri ameingia katika headlines baada ya kuonesha nia ya dhati ya kutotaka kuichezea Ufaransa tena.

2B9B216500000578-3261803-image-a-77_1444129500101

Samir Nasri ambaye amenukuliwa akisema hawezi kuichezea timu ya taifa ya Ufaransa hata kama baba yake mzazi angechaguliwa kuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Samir Nasri ambaye amewahi kuichezea timu ya taifa ya Ufaransa ya wakubwa kuanzia mwaka 2007 hadi 2013, alitangaza kustaafu soka kuichezea Ufaransa August 2014 baada ya kocha wa Ufaransa Didier Deschamps kumuacha katika kikosi cha Ufaransa kilichocheza Kombe la Dunia 2014.

2CE5B55700000578-3261803-image-m-82_1444129675572

“Hata kama baba yangu akichaguliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa siwezi kurudi kuichezea, nimeangaika kucheza vizuri ili nichachaguliwe timu ya taifa lakini nikakosa Kombe la Dunia 2014, Mpango wangu ulikuwa ni kustaafu timu ya taifa toka 2012 ila baba yangu alinishauri nicheze kombe la Dunia 2014 kwa sababu nilikuwa na kiwango kizuri”>>> Nasri

Samir Nasri amewahi kuichezea timu ya taifa ya Ufaransa michezo 41 na kufunga magoli 5 katika kipindi cha mwaka 2007-2013, ameoneshwa kuudhunishwa na tukio la kuachwa kwake katika kikosi kilichocheza Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil. Nasri amejibu hayo baada ya kuulizwa kama anaweza kurejea kuichezea Ufaransa. Sababu za kuachwa kwa Samir Nasri katika Kombe la Dunia 2014 zinatajwa kuwa sio za kushuka kiwango ila ni tofauti zake Didier Deschamps.

2CF97C7100000578-3261803-image-a-83_1444129715120

Didier Deschamps.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE

Tupia Comments