Vituo vya mitandao ya kijamii vinavyohusishwa na Kundi la Wagner la Urusi vinasema mpiganaji wa ngazi ya juu alizuiliwa nchini Finland kwa ombi la Ukraine.
Mtu huyo alitambuliwa kama Yan Petrovsky, ambaye amepigana nchini Ukraine tangu 2014 kama sehemu ya Rusich, au Kundi la Upelelezi wa Mashambulio ya Sabotage, kitengo kidogo cha Wagner.
Alikamatwa mwezi mmoja uliopita na sasa anaweza kurejeshwa kwa Ukraine, kulingana na kituo cha Telegram.
Mahakama ya wilaya ya Vantaa karibu na Helsinki inatarajiwa kuongeza muda wa kuzuiliwa kwa Petrovsky kwa ombi la Ofisi ya Kitaifa ya Upelelezi ya Finland, afisa wa mahakama alisema.
Ofisi hiyo ilitaka kuzuiliwa kwa Petrovsky, ambaye pia anatumia jina la Voislav Torden, kwa tuhuma za kushiriki na kuunga mkono ‘ugaidi’, afisa huyo alisema.