Habari za Mastaa

Davido alivyokiamsha kwenye stage ya Hot 97 na Cardi B, Meek Mill (+Video)

on

Jumapili ya June 2,2019 mkali kutokea Nigeria Davido alitoa burudani kwenye stage ya Hot 97 katika tamasha la Summer Jam 2019 lillilofanyika Marekani, Davido alipata nafasi ya kutumbuiza kwenye show hiyo kubwa na wakali kama Cardi B, Meek Mill, Migos, Tory Lanez, Rich The Kid na wengine kibao.

Inaelezwa kuwa ili kupata tiketi ya kuwaona wakali hao juu ya stage ilipaswa mtu wa kawaida kulipia kiasi cha thamani ya dola za Kimarekani 234 ambayo ni  sawa na zaidi ya shilingi laki tano za Kitanzania, hata hivyo ngoma ya ‘Fall’ ilitajwa kuwa ndio wimbo wa kwanza kutoka kwa msanii wa Nigeria kuwahi kukaa muda mrefu zaidi kwenye chart za Billboard ukilinganisha na nyimbo nyingine za Afrobeats ambazo ziliwahi kukaa kwenye chart hizo.

January 28,2019 iliripotiwa Davido alishika nafasi ya pili kwa ujumla kuujaza uwanja wa O2 mjini London Uingereza baada ya Wizkid na amevunja rekodi ya kuwa msanii wa kwanza mwenye umri mdogo kutokea katika Bara la Afrika kuujaza uwanja huo.

VIDEO: KUELEKEA NANDY FESTIVAL, WASANII SUMBAWANGA WAONESHA UWEZO WAO

Soma na hizi

Tupia Comments