Habari za Mastaa

Navy Kenzo, Joh Makini Gnako kwenye Stage Moja na Burna Boy DSM

on

Siku ya Ijumaa November 29, 2019 linatarajiwa kufanyika tamasha la muziki litakalo mdondosha mkali kutokea Nigeria Burna Boy ambaye atafika Tanzania kwa mara ya kwanza kwaajili ya kufanya show ambapo kwenye stage ataungana na wasanii wa muziki wa Bongo Fleva ambao ni Joh Makini, Gnako pamoja na kundi la Navy Kenzo.

Wasanii hao wa Bongo Fleva watakao panda kwenye stage moja na Burna Boy wamejigamba kuwa watamkalisha msanii huyo wa Naigeria kwenye tamasha hilo linatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Next door Arena Jijini Dar Es Es Salaam.

“Tunajisikia furaha kuwa miongoni mwa wasanii tutakao toa burudani pale, na hii itakuwa mara yetu ya pili kuperform same stage na Burna Boy maana kuna kipindi tuliperfom SA na sasa hivi tunamkaribisha hapa nyumbani, Tunamkaribisha kila mtu na kama unavyojua mahali walipo Navy Kenzo lazima moto uwake”  – Nahreal

“Mimi Binafsi najisikia kuheshimiwa lakini pia naona muziki wa Hip Hop umeheshimiwa, uwakilishi wangu kwenye hili tamasha kama msanii wa Hip Hop nabeba jukumu zima kwasababu hii ni show ya kimataifa na Burna Boy ni msanii mkubwa na hata sisi ni wasanii wa kimataifa, kwahiyo ambacho tunakwenda kufanya pale Next Dor Arena siku ya ijumaa ni kuhakikisha hata Burna Boy mwenyewe tunamuachia alama atajua kama alikutana na kina Joh Makini” – Joh Makini

CASTO KAMJIBU TUNDA BILA UWOGA “WEWE NI VIDEO VIXEN TU UNAKUJA KUNIAMBIA NINI, MESSAGE ZA KUEDIT”

Soma na hizi

Tupia Comments