fB insta twitter

#Goodnews Navy Kenzo watangaza collabo na kundi hili la muziki kutoka Ghana!

on

Kila kitu kinachoguswa na kundi la muziki kutoka Tanzania, Navy Kenzo lazima kiwe ‘Above In A Minute’… yes mtu wangu kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa muziki wa Navy Kenzo utakubaliana na mimi kwenye hili.

Good news kwako shabiki wa muziki wa Bongo Fleva, kundi la Navy Kenzo linaloundwa na Producer Nahreel na mpenzi wake Aika limeshare na sisi kupitia page yao ya Instagram ujio wa collabo mpya na  kundi la muziki kutoka Ghana, R2bees!

KENZOGHANA

Navy Kenzo, Victoria Kimani, Wizkid, Vanessa Mdee, Patty Monroe na DJ. Spinall.

Kupitia official Instagram page ya kundi la Navy Kenzo @navykenzoofficial, wamepost picha na caption inayosema…

>>> “Wazee wa slowdoown @r2beesmusic straight kutoka Ghana kaa mkao wa lolote kubwa kutokea baina ya Navy Kenzo feat @r2beesmusic. Unaweza kisia nyimbo itakuwa ya miondoko gani???? #AboveInAMinute #AfricanMusicConcert2015 #GameGame #Nipendelee.” <<< @navykenzoofficial.

KENZOGHANA2

Kundi la R2bees kutoka Ghana linaundwa na ndugu wawili, Faisal Hakeem maarufu kama Paedae da Pralem na Rashid Mugeez maarufu kama Mugeez… kundi hilo pia limeshawahi kunyakuwa tuzo kubwa za kimataifa ikiwemo BET Awards 2013 ‘Best International Act: Africa na kwa upande wa tuzo za nyumbani, R2bees wanashikilia tuzo 9 za Ghana Music Awards.

KENZOGHANA3

Navy Kenzo walikuwa Johannesburg, South Africa kwa ajili ya kuperform kwenye tamasha la African Music Concert maarufu kama AMC 2015, na baadhi ya wasanii waliohudhuria tamasha hilo ni pamoja na mtu wetu Vanessa Mdee,Wizkid, Davido, AKA, Victoria Kimani, Runtown na wengine kibao.

Hapa chini nimeisogeza moja ya kazi za R2bees kutoka Ghana, kuinasa bonyeza play hapa chini.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments