Rapper Nay wa Mitego amefika baraza la Sanaa la Taifa BASATA leo hii, baada ya kupokea wito na baada ya kufika alipewa barua iliyoainisha makosa aliyofanya kupitia wimbo wake wa ‘Nitasema’
Barua hiyo ambayo imewekwa hadharani na mwanssheria wa Nay wa Mitego akidai wameipokea kutoka BASATA imeainisha makosa manne ambayo ni kutoa wimbo kwa walaji bila kibali, kutoa wimbo maudhi yake yanahamasisha uchochezi, wimbo wenye maudhui yanayokashifu mataifa mengine na Wimbo ambao maudhui yake yanapotosha jamii, na katika makosa hayo kila kosa Lina maelezo yake huku barua hiyo Ikiwa imetolewa na Ndug Buganga huku nakala ikienda kwa Katibu mtandaji Dkt Mapana
tazama zaidi…