Habari za Mastaa

Nay wa Mitego kamalizana na BASATA lakini……

on

Kama utakuwa unakumbuka 27, 7, 2016 Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) lilitoa tamko la kumfungia msanii wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego kutojihusisha na kazi ya sanaa kwa muda usijulikana

Sasa leo August 15, 2016 baraza hilo limetoa tamko rasmi la kumfungulia msanii huyo kufanya kazi ya muziki huku akiwa kwenye uangalizi maalum sehemu ya kuhakikisha anaendesha shughuli za sanaa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu na kuzingatia maadlili katika kazi zake.

Kwa mujibu wa Katibu mkuu wa BASATA Godfrey L. Mngereza aliyaongea haya>>>>Itakumbukwa kwamba mnamo tarehe 27/7/2016 Baraza lilimfungia Msanii Nay wa Mitego  kwa kipindi kisichojulikana na kumtaka kutekeleza maagizo yafuatayo:AW1A4757

1.Kuhakikisha amesajiliwa na kuwa na kibali cha kuendesha shughuli za Sanaa

2.Kulipa faini ya Shilingi milioni moja (1,000,000/-)

3.Kuomba radhi watanzania kupitia mkutano wa waandishi wa habari na kwenye akaunti  zake za mitandao ya kijamii

4.Kuufanyia marekebisho wimbo wa ‘Pale Kati’ ili ubebe maudhui yenye maadili

Msanii huyo ametekeleza adhabu zote zilizotajwa hapo juu, hata hivyo pamoja na kuleta marekebisho mara mbili ya wimbo wa ‘Pale Kati’ Baraza bado halijaridhishwa na marekesho hayo hivyo linaendelea kuufungia wimbo huo hadi hapo litakapojiridhisha umekidhi vigezo vya kimaadili‘- Godfrey Mngereza

BASATA  limetoa agizo kwa msanii huyo kuendelea kuufanyia marekebisho wimbo wake huo kama bado atakuwa anauhitaji

ULIIKOSA  HII YA NAY WA MITEGO KUHUSU KUMALIZANA NA BASATA BASI ISIKILIZE HII SAUTI HAPA

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments