Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Mahakama nchini Sweden yamkuta na hatia Asap Rocky

on

Inaripotiwa kuwa Mahakama nchini Sweden imemkuta na hatia rapper Asap Rocky na wenzake wawili kwenye kesi iliyokua ikimuandama  ya kumpiga na kumjeruhi shabiki mmoja nchini humo ambapo ishu hiyo ilitokea 30 June,2019.

Inaelezwa kuwa Mahakama imeamua kutompa kifungo cha jela na kuamuru kuwa itabidi amlipe  fidia ya kiasi cha shilingi Milioni 3 za Kitanzania kijana huyo kutokana na kumjeruhi hata hivyo imeripotiwa kuwa Mahakama imeamua kufanya hivyo kutokana na kudai kuwa Asap alisota rumande kwa muda na ugomvi huo haukusababisha maafa makubwa ya kufikia hatua ya kumpa kifungo.

Rais Donald Trump aliwahi kuingilia kati kuhusu kesi hiyo huku wasanii wenzake Asap Rocky walipaza sauti ili aachiwe huru akiwemo Snoop Doggy na baadae Kim Kardashian alifikisha maombi yake kwa Trump na kuelezwa Asap angehukumiwa kifungo cha miaka 6 jela.

VIDEO: FID Q AKIZUNGUMZANA WAANDISHI WA HABARI WAKATI WA UZINDUZI WA ALBUM YAKE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA 

Soma na hizi

Tupia Comments