Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

DJ Black Coffee ajivunia kukutana hadi kushikwa mkono na Drake (+video)

on

Mwimbaji na Dj maarufu kutokea Afrika Kusini Black Coffee amezungumza kupitia ukurasa wake wa instagram jinsi gani alivyojawa na furaha mara baada ya kukutana na rappa Drake kutokea Canada ikiwa kama moja ya kukamilisha ndoto zake.

Black Coffee ambaye jina lake halisi ni Nkosinathi Innocent Maphumulo alizidi kumiminika kupitia video hiyo na kusema kuwa alihisi kuwa endapo angekutana na rapper huyo basi angekua chizi lakini alishangaa alishikwa mkono na Drake na kuitwa Mkongwe (Legend), Black Coffee alisema kuwa endapo atapata nafasi ya kukutana na Steven Wonder ataangusha machozi.

Black Coffee alipata umaarufu mkubwa mwaka 2005 baada ya kushinda tuzo ya SAMA Best Urban Dance Album na mwaka 2015  alishinda tuzo ya “Breakthrough DJ of the Year” katika tuzo za djs zilizofanyika Ibiza, aliwahi pia kuachia ngoma kama Your Eyes, Turn Me On, Muye, Juju na nyingine nyingi.

“Nilivyokutana na Drake nilijua nitapoteza akili zangu lakini alikuja na kuchukua mkono wangu na kuushika na kusema Mkongwe” nahisi nimekutana na kila mtu ambae nilitaka kukutana nae kasoro Steve Wonder nahisi ikitokea nikikutana nae nitalia” >>> alisema Black Coffee.

 

AUDIO: UMEPITWA NA HII YA WEMA SEPETU KUPELEKWA GEREZANI SIKU 7? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA MWANZO MWISHO 

Soma na hizi

Tupia Comments