Muda mfupi baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, kuagiza Jeshi la Polisi kumuachia huru Msanii Nay wa Mitego ambaye alikuwa akishikiliwa na Jeshi hilo kwa tuhuma za wimbo wake wa ‘WAPO’ kutokuwa na maadili, Nay wa Mitego ametoka kituoni hapo leo March 27 2017.
Msanii Nay wa Mitego akitoka kituo cha polisi kati ikiwa ni muda mfupi baada ya agizo la Waziri Mwakyembe kutaka aachiwe huru pic.twitter.com/k1EWzlrYju
— millardayo (@millardayo) March 27, 2017
'Asante kwa wote walioamka na kuwa upande wangu, upande wa haki, walioamini kile ambacho nimekifanya nawashukuru sana'-Nay wa Mitego pic.twitter.com/kbtHHz7rcV
— millardayo (@millardayo) March 27, 2017
VIDEO: Uliikosa hii ya Serikali kuliagiza Jeshi la Polisi kumuachia Nay wa Mitego na kuruhusu wimbo wa ‘Wapo’? Bonyeza play hapo chini kutazama.