Videos

Ruby kawa tayari kutuletea Video yake ya Na Yule,itazame hapa kwa mara ya kwanza mtu wangu..

on

ruby ingine

Ni single ambayo ilizaliwa wakati tukielekea kwenye mbio za Valentine mwaka 2015,uzito wa maneno yaliyomo kwenye wimbo huu umeufanya kuendelea kushika nafasi za juu kwenye chart mbalimbali za radio Tanzania.

ruby og

Mei 15 kaamua kuipa heshima kwa kuachia video yake ambayo imeongozwa na Director kutoka Kenya anaitwa Kelvin Bosco JNR ambaye tayari amefanya video kadhaa za mastaa wa Tanzania  ikiwemo Akadumba ya Ney wa Mitego,Asante ya AY,Mfalme ya Mwana Fa  na zingine kibao.

Huyu anaitwa Ruby msichana ambaye alizaliwa kupitia mashindano ya Serengeti Super Nyota Diva 2014,hii ni video ya single yake mpya Na yule,itazame hapa mtu wangu.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufiki

Tupia Comments