Premier Bet SwahiliFlix Ad Vodacom Ad

Habari za Mastaa

Drake adaiwa kuiba wimbo wa ‘In My Feelings’

on

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Rapper Drake amefunguliwa shtaka la kuiba mdundo wa ngoma ya ‘In My Feelings’ na msanii Samuel Nicholas III bila ruhusa kwenye ngoma yake halali ya ‘Roll Call’ na kudai kuwa hakulipwa chochote na rapper huyo.

Ngoma ya ‘In My Feelings’ iliachiwa rasmi August 3,2018 katika mtandao wa You Tube ambapo mpaka sasa imetazamwa na jumla ya watu Mil.200 huku Samuel Nicholas III akitoa malalamiko kuwa aliutoa wimbo wake wa ‘Roll Call’ mwaka 200 na kudai kuwa Drake aliiba tena mdundo mwingine kutoka kwake na kuutumia kwenye ngoma iliyofanya vizuri ‘Nice For What’.

Kwa mujibu wa  nyaraka zilizohifadhiwa na TMZ zimedai kuwa Samuel aliweka ngoma yake ya ‘Roll Call’ kwa mfumo wa CD mwaka 2000 na hakujua mdundo wake umetumika kwenye ngoma ya ‘In my Feelings’ mpaka baada ya muda ndipo alipogundua baada ya kuona ngoma hiyo ikipanda kwenye charts za ngoma zilizofanya vizuri.

Hata hivyo imeelezwa kuwa kwenye shauri hilo mwimbaji huyo Samuel Nicholaus III amejumuisha record label ya Republic Records, Asylum Records na Cash Money, imeripotiwa kuwa wamejaribu kuwasiliana na Drake lakini yup kimya.

VIDEO: CHUCHU KAWAJIBU WANAOMJADILI YEYE NA RAY ‘MANENO HAYANIUMIZI NAFANYA NACHOTAKA’ 

Soma na hizi

Tupia Comments