Michezo

Huyu jamaa kachukua record ya urefu wa Hasheem Thabeet Ligi ya NBA…

on

Hasheem

Hasheem Thabeet, picha na #SlideVisual.

Hasheem Thabeet jina la kwanza la Mtanzania kuingia kwenye Headlines Duniani akitajwa kama Mbongo wa kwanza kuchezea Ligi ya Mpira wa Kikapu Marekani, NBA.

Sim Bhullar unaambiwa ni jina jingine kubwa TENA kuingia kwenye NBA.. Jamaa hatokei BONGO, ni raia wa Canada ambaye tayari kasaini contract ya siku 10 na timu ya Sacramento Kings.. wazazi wake wana asili ya India, baadae walihamia Canada ambapo Bhullar alizaliwa mwaka 1992, hivyo anakuwa mchezaji wa kwanza ambaye ana asili ya India kuchezea Ligi ya NBA.

sim1

Sim Bhullar.

Bhullar ana urefu wa futi 7.5, anakuwa mchezaji wa kwanza kwa urefu kwa sasa hivi, anampita Hasheem Thabeet ambaye ana futi 7.3.

manute-bol-e1339178761329

Manute Bol, aliyenyoosha mikono katikati.

Hasheem na Bhullar ni warefu, lakini rekodi ya mchezaji mrefu zaidi aliyewahi kuchezea NBA bado inashikiliwa na Manute Bol, alikuwa raia wa Sudan alikuwa na urefu wa futi 7.7, alifariki kwa ugonjwa wa ini mwaka 2010.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments