Leo May 5, 2017 kupitia Clouds 360 ya Clouds TV msanii wa sanaa ya michoro ya vibonzo ‘katuni’ kwenye magazeti Nathan Mpangala amesema kuwa lengo la kazi hiyo ni kuwasilisha ujumbe kwa jamii na kufurahisha.
Nathan Mpangala ambaye ameanza rasmi kuchora vibonzo zaidi ya miaka 15 iliyopita anajulikana zaidi kupitia vibonzo kama vile Mtu kwao, Mzungu mtaani Manyusi na vinginevyo akisema kuwa kazi hiyo inalenga kuwasilisha ujumbe na kufurahisha
“Nimechora vibonzo vingi sana Mtu Kwao, Mzungu, Mtaani, Manyusi na vibonzo vingine vingi. Nilianza mwaka 1998 mpaka sasa nina miaka zaidi 15 ndani ya uchoraji.
“Katuni ni chombo cha mawasiliano ambacho moja ya kazi yake ni kufikirisha na kukufanya ucheke. Kuna aina tofauti za uchoraji, inategemea na mchoraji. Kwa mimi nilisomea Fine Art.” – Nathan Mpangala.
Baadhi ya katuni alizowai kuchora mchoraji Nathan Mpangala
VIDEO: Maamuzi mapya ya Asley baada kukabidhiwa wasanii sita…