Jeshi la polisi nchini kupitia kwa msemaji wake mratibu mwandamizi Advera Bulimba limetoa onyo kwa wananchi waliojipanga kufanya uhalifu katika kipindi cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.
Akiongea na waandashi Dar es salaam mratibu mwandamizi Advera Bulimba amesema…>>>’Tunaelekea katika kipindi cha mwisho wa mwaka ambapo kuna sikukuu za kufululiza lakini katika uzoefu tumeona ni muda ambao baadhi ya watu wamekuwa wakitumia fursa zilizopo‘
‘Lakini pia wapo baadhi ya watu wamekuwa wakitumia nafasi hizo kwa ajili ya kufanya uhalifu ikiwa ni pamoja na wale wanaojipatia kipato kisicho halali‘ –Advera Bulimba
‘Jeshi la polisi tumejipanga vyema na hatutaruhusu mtu yeyote aharibu amani ya nchi kwa sababu zake binafsi, tunaomba wananchi watoe ushirikiano wa kutosha katika kushiriki ulinzi shirikishi‘ –Advera Bulimba
Unaweza kuendelea kumsikiliza mratibu mwandamizi Advera Bulimba kwenye hii video hapa chini…
EXCLUSIVE: ‘Ukweli sina mimba, nilifanya vile kwa sababu’ Nisha