Moja ya headline zilizochukua nafasi kuanzia usiku wa August 23 2016 ni pamoja na tukio la mauaji ya Askari Polisi wanne katika shambulizi lililofanywa na majambazi katika Bank ya CRDB Mbande, Dar es salaam.
Leo August 25 2016 baadhi viongozi wa Serikali akiwemo Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda wameungana na watanzania wengine kuaga miili hiyo ya marehemu.
Hapa nakukutanisha na Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba aliposimama kuongea na waombolezaji ambapo pia ametaka wale wote walioshiriki kuandika mambo ya kufurahishwa katika tukio hilo wakamatwe.
ALICHOKISEMA WAZIRI NCHEMBA BAADA YA KUFIKA ENEO WALIPOUAWA ASKARI POLISI DAR