Top Stories

Ndani ya daladala:binti kabakwa, kapigwa na kuporwa fedha “gari ilibadili njia”

on

Jeshi la Polisi mkoani Arusha linawatafuta watu watatu ikiwemo dereva na kondakta wa moja ya daladala mkoani Arusha  kwa kutuhumiwa kumpiga,kumuibia simu pamoja nakumbaka binti ambaye alikuwa anatoka kazini baada yakubadilisha njia nakumpeleka sehemu nyingine.

Binti huyo amedai  alikuwa akitoka kazini usiku maeneo ya Field Force katika kata ya Murieti kuelekea kontena na baada yakupanda daladala hiyo walibadilisha njia

“walifika sehemu kuna migomba mingi wakasimamisha gari,nikaruka nikakimbia akanikimbiza mmoja akanipiga akaniingiza kwenye migomba akaniambia nivue nguo nikakataa akaanza kunipiga mwisho wa siku wenzake wakaja wakanizidi nguvu wakanivua nguo wawili wakanibaka,wakachukua begi hela na simu zote mbili”

 

MOTO WAZUKA GHAFLA KWENYE GARI WAKATI DEREVA AKIBADILISHA TAIRI “NILITOKA MOMBASA”

Soma na hizi

Tupia Comments