Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa Bilioni 12 ndani ya miezi minne katika mradi wa Ujenzi unaounganisha Kilometa 345 ya Makao Makuu ya Mkoa wa Arusha na Wilaya ya Ngorongoro.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela akiongozana na kamati ya siasa ya Mkoa wa Arusha wametembelea ujenzi huo utakaogharimu billion 87.1.
“Ndani ya miezi hii minne Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ametoa takribani Bilioni 12 kwaajili ya mradi huu wa Barabara, ambayo imewezesha haya yote mliyoyakagua”– RC Arusha
ASKOFU GWAJIMA NA JERRY SLAA WAITWA KAMATI YA MAADILI BUNGENI “KUJIBU TUHUMA IKIWEMO KUSEMA UONGO”