Michezo

Ndani ya wiki Mayweather apoteza wawili muhimu

on

Bondia Floyd Mayweather wa Marekani huu umeendelea kuwa wakati mgumu kwake kutokana na kuendelea kupata pigo ndani ya muda mfupi.

Leo Mayweather ameripotiwa kumpoteza mjomba wake Roger Mayweather  ambaye ni mtu muhimu sana katika maisha yake ya boxing kwani ndiye aliyekuza kipaji chake.

Roger aliyefariki akiwa na umri wa miaka 58 amepoteza maisha kutokana na maradhi ya kisukari na afya yake kuwa dhaifu, huu ukiwa ni msiba wa pili unampata Floyd Mayweather ndani ya wiki baada ya kufiwa na mama watoto wake Josie Harris aliyezaa nae watoto watatu.

 

Soma na hizi

Tupia Comments