Duniani

PICHA 4:Ndege yenye kasi zaidi duniani kutengenezwa, Australia hadi Marekani zitatumika saa sita

By

on

March 28, 2017 millardayo.com inakusogezea story inayoihusu Kampuni ya Boom Supersonic’s XB-1 ambayo imeanza kutengeneza ndege ya kwanza yenye kasi zaidi duniani ambayo itaweza kumsafirisha mtu kutoka Bara la Australia mpaka America ya Kaskazini kwa muda wa saa sita tu.

Utengenezaji wa ndege hiyo utagharimu zaidi ya Dola million 329 za Marekani na inatarajia kukamilika mwaka 2020 ambapo CEO wa kampuni hiyo Blake Scholl aliiambia Daily mail kuwa ndege hiyo itakuwa na uwezo wa kuruka umbali wa zaidi ya futi 60,000 kutoka usawa wa Bahari ambao ni umbali mrefu sana ukilinganisha na ndege za kawaida.

Ndege hiyo itakuwa na kasi zaidi ya Concord ambayo inajulikana kama ndege yenye kasi zaidi duniani na itakua na seat 45 na safari zake zitagharimu Dola 6,600 za Marekani na itaweza kumsafirisha mtu kutoka Japan mpaka San Francisco kwa muda wa saa tano tu wakati ndege ya kawaida husafiri kwa zaidi ya saa 10 na dakika 48.

 

VIDEO: Vipi ulimiss hii stori kuhusu bilionea kutoka Tanzania? Nimekusogezea hapa bonyeza play kutazama.

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

Soma na hizi

Tupia Comments