Mix

Ukaaji huu kwenye ndege ilikuwa tatizo kwa mtu wa pembeni, mambo yamebadilika.. Kilichofuatia je??

on

etihad

Kampuni ya ndege ya Etihad iliyopo Abu Dhabi imeingia kwenye headlines baada ya abiria James Bassos kuishitaki kampuni hiyo kwa matatizo ya mgongo yaliotokana na kupangiwa siti karibu na mtu mnene.

etihad2

Documents zilizopelekwa Mahakamani na James Bassos zina maelezo kwamba wakati akiwa safarini kutoka Dubai kwenda Sydney mwaka 2011 alilazimika kujigeuza geuza na kujibana ili kuzuia kugusana na mwenzake ambae mwili na uzito wake ni mkubwa kupita kiasi.

Licha ya kuomba kuhamishwa siti zaidi ya mara moja na wahudumu wa ndege hiyo, ombi lake ni kama hakuna aliyejali kumsaidia zaidi ya kumpa ushauri kwamba kama akijisikia maumivu ainuke kujinyoosha nyoosha kidogo !!.. badaae akashuka akiwa na maumivu makali sana ya mgongo.

James-Bassos-665x385

Kesi hiyo dhidi ya ETIHAD bado inaendelea lakini kama Kampuni hiyo ya ndege ikikutwa na hatia basi kampuni hii itakuwa imevunja sheria kuu ya kampuni yao inayosema “usalama na faraja ya abiria wa Etihad Airways ni suala la umuhimu kwetu…”

Kampuni ya ETIHAD hii ni mara ya pili inaingia kwenye headlines zisizopendeza, ni April 2015 walitajwa kumfukuza kazi mfanyakazi mwanamke mmoja kwa sababu alikuwa mjamzito !!

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments