Mtu wangu naamini utakua unakumbuka jinsi ajali za ndege zilivyochukua headlines miaka michache iliyopita, hali hiyo imefanya makampuni ya usafirishaji wa ndege duniani kuboresha huduma zao kwa kununua ndege za gharama na imara ili kuweka ushindani wa kibiashara na kuongeza usalama kwa wateja wao. Mpaka sasa usafiri wa ndege ndio pekee unaotajwa kuwa salama zaidi kuliko usafiri wa aina nyingine yeyote.
Ripoti iliyotolewa na JACDEC Airline Safety Ranking 2016, imezitaja kampuni 60 za ndege zenye usalama zaidi duniani. Leo nakuletea Top 10 ya kampuni hizo mtu wangu. JACDEC inasimama badala ya Jet Airliner Crash Data Tathmini Centre, ambao hutoa uchambuzi juu ya usalama wa kimataifa kwenye biashara za anga tangu 1989.
10. TAP Portugal
Hii ni kampuni ya usafirishaji kutoka Ureno, imekamata nafasi ya 10 ikifatana na kampuni ya Japan Airlines. TAP wameshikika nafas hii baada ya kuongeza idadi ya ndege kubwa pamoja na kupewa kibali cha kuongeza safari zao ambazo zinafikia asilimia 75 ya viwanja wanavyotua kila siku duniani. Uwezekano wa ndege zao kupata ajali ni 0,015 unaowaweka kwenye nafasi ya 10 ya ndege salama duniani.
Japan Airlines sio tu ni salama, hawa wana sifa nyingine nzuri, kufanya kazi zao on time. Mwaka 2015 walipewa tuzo ya kufikisha aslimia 89.44% ya ndege zao kufanya safari ndani ya muda uliopangwa, na kuwa ndege za kwanza barani Asia na upande wa Pacific kuweka rekodi hiyo. Ulinzi pia imetajwa kama sifa yao kubwa, Uwezekano wa ndege zao kupata ajali umetajwa kuwa 0.015 kwa mwaka 2016 kinachowaweka kwenye nafasi ya 9.
Hii ni kampuni kutoka Abu Dhabi ambayo slogan yao ni “From Abu Dhabi to the World”. Etihad inafanya safari zakr kwenye mabara matano kati ya saba duniani. Kampuni hii imefungua pia chuo cha marubani ambako kinawatrain wanafunzi ili kupata marubani wapya siku za usoni watakaofanya kazi kwenye ndege za umoja wa falme za kiarabu. Uwezekano wa ndege zao kupata ajali ni kwa asilimia 0.013.
Kwanza ndio kampuni ya ndege pekee duniani zenye rangi nyeusi ikiwa na safari zake kwenye miji ya Osaka, Houston na Vietnam, huku wakishirikiana na Trans-Tasman, Air China, Singapore pamoja na United Airlines ili kusafiri kwenye nchi nyingi zaidi. maeneo ambayo wanafanya safari nyingi zaidi ni Adeline, Melbourne, Sydney na Tasmania huko Australia, pamoja na Bali. Uwezekano wa ndege zao kupata ajali ni asilimia 0.011 kwa mwaka 2016, hii inawafanya washike nafasi ya 7 kwenye list ya ndege salama zaidi duniani.
6. KLM
Moja kati ya brands kubwa kutoka nchini Uholanzi: KLM Royal Dutch Airlines. Inafanya safai zake Ujerumani, ndani ya Uholanzi, Norway, nchi za Ulaya pamoja na Marekani, ni moja kati ya kampuni kongwe kwenye usafiri wa ndege duniani, KLM ilianzishwa October 7, 1919, na wanakaribia kufikisha miaka 100 ya kutoa huduma za usafiri wa ndege. Hii inakamata nafasi ya 6th ikiwa na uwezekano wa ndege zake kupata ajali kwa asilimia 0.010, imefungamana na Hainan Airlines.
Sifa kubwa ya Hainan Airlines ni kutunza utamaduni wa nchi yao, hawa wanatokea Japan, basi hata wahudumu wake muda wote wanakua wamevalia mavazi yenye utamaduni wa Kijapan. Pia muonekano wa ndani ya ndege zao zote umenakshiwa kwa mapambo ya Kijapan. Hainan inafanya safari zake kwenye nchi za Marekani, Canada, Ubelgiji, Ujerumani, Ufaransa, Umoja wa Ulaya, Italia, Jamhuri ya Czech, Urusi, Kazakhstan, Israel, China, Taiwan, Japan, Hong Kong, Thailand na Australia. Iko nafasi ya 5th ikiwa na uwezekano wa kupata ajali kwa asilimia 0.010 ya viwango vya usalam wa ndege.
Qatar Airways ilianzishwa miaka 25 iliyopita. Na ilianza safari zake mwaka 1994 ikiwa inamilikiwa na familia ya kifalme ya Catari. Kampuni hii inamiliki brands nyingine nyingi za ndege ikiwa ni pamoja na hisa kubwa zaidi za uwanja wa ndege wa Doha, The International Airport of Doha. Kazi yao nzuri imewaweka kwenye naffasi ya 4th wakiwa na morali ya kupanda zaidi siku zijazo. Uwezekano wa ndege zao kupata ajali ni asilimia 0.009.
Kampuni ya Hello Kitty ndio wamiliki wa Eva Air. Ni kampuni ya Kijapan ambayo iko tofauti sana kwenye ndege zake zote, kila ndege ya kampuni hii imegawanywa sehemu ya kukaa watoto peke yao na wanapewa midoli huku sehemu za kukaa watu wazima kuna specila treatment ya nyama na mboga mboga. Hii iko nafasi ya 3 na uwezekano wa ndege zake kupata ajali ni asilimia 0.008.
2. Emirates
Inafahamika pia kama Fly Emirates. Asili yake ni Dubai, na inamilikiwa na serikali ya United Arab Emirates. Hii ina sifa kubwa kutoa huduma kwa kiwango cha kifalme na ifanya safari zake kwenye viwanja zaidi ya 150 katika mabara 6. Uwezekano wa ndege zake kupata ajali ni chini ya asilimia 0.007, na wanapambana kumantain au kupanda zaidi kwenye nafasi ya pili.
Hii ni kampuni kutoka Hong Kong na inafanya safari zake kutoka Hong Kong kwenda, Taipei, Bangkok na Singapore. Kitu cha kipekee kwenye ndege hizi ukiwa mteja wa mara kwa mara unapewa Club Membership Card ambayo inakufanya uweze kupata huduma za starehe bila malipo ya ziada. Imetajwa kwenye nafasi ya 1 huku kiwango cha uwezekano wa ajali ni mdogo kufikia 0.006.