Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi amesema Serikali itafanya mabadiliko makubwa kwenye nafasi za Maafisa Utumishi kama Maafisa hao wataendelea na tabia yao ya kushindwa kupeleka majina ya watumishi wenye sifa za kupandishwa madaraja.
Ndejembi ametoa kauli hiyo leo alipokutana na kuzungumza na Watumishi wa Halmashauri mbili za Wilaya ambazo ni Kondoa Mji na Kondoa Vijijini ambapo amesisitiza kuondoa migogoro na migongano kwenye maeneo ya kazi.
” Maelekezo ni kwamba maafisa utumishi wote Nchi nzima kuhakikisha wanatenda haki, kila mtumishi anaestahili kupandishwa daraja kwa maelekezo ya Rais Samia basi apate haki yake. Tutamchukulia hatua Afisa Utumishi yeyote ambaye atakua kikwazo cha watumishi wenye sifa kushindwa kupanda cheo” Naibu Waziri Ndejembi.
“Tuondoe migongano kwenye maeneo ya kazi, siyo unakuta watumishi hawa wa Mkuu wa Wilaya hawa wa Mkurugenzi wa Halmashauri, hatuzuii watu kuwa na mahusiano lakini yasizidi kiasi cha kuwa chanzo cha kuharibu kazi na kufanya Serikali ionekane haifanyi kazi,” Naibu Waziri Ndejembi.