Breaking News

BREAKING: Mume wa zamani wa Irene Uwoya Ndikumana amefariki, chanzo chatajwa na alichoomba kabla ya kufariki

on

Asubuhi ya leo Tanzania imezipokea taarifa za kifo cha aliyekuwa Kocha msaidizi wa timu ya Rayon Sports ya Rwanda, Hamad Ndikumana Katauti ambae amefariki ghafla.

Mwandishi wa habari za Michezo Shaffih Dauda ameripoti kwamba Gakwaya Olivier ambae ni Afisa Habari wa Timu hiyo amesema Ndikumana amefariki kwa kile kinachosadikiwa kuwa ni ugonjwa wa moyo.

“Alisikia maumivu makali kifuani akaomba soda ya baridi wakamletea na alipomaliza kunywa tu kidogo akatapika na akaishiwa pumzi na ndipo akakata kauli, bado tunasubiri uchunguzi wa kina wa kitabibu”

Marehemu aliwahi kucheza soka Tanzania akiwa na Stand United na ni Mume wa zamani wa  Mwigizaji Irene Uwoya na wana mtoto mmoja. RIP Ndikumana

ULIPITWA? HII NI VIDEO YA LULU AKIPELEKWA GEREZANI BAADA YA HUKUMU, PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

VIDEO: IRENE UWOYA AFUNGUKA KUHUSU MWANAMKE ATAEMCHUKULIA MWANAUME WAKE… PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA

EXCLUSIVE VIDEO: DR. LUIS SHIKA AONGEA BAADA YA KUTOKA POLISI, “WHAT DO THEY MEAN?” MTAZAME HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments