Premier Bet
TMDA Ad

Duniani

Sababu za kwanini Wanandoa wengi hufanana

on

Ni miongoni mwa swali wanalojiuliza watu wengi kwanini Wanandoa wengi hufanana? sasa leo nimekuletea majibu ambapo Wanasayansi wa chuo kikuu Boston Marekani wamefanya uchunguzi na kugundua sababu kubwa ya wanandoa kufanana ni kuoa watu wanaoshea historia ya undugu mfano watu wa kabila moja.

Rapa Dj khalid na mke wake Nicole Tuck

Wanasayansi hao wamesema kitendo cha watu kwenda kuoa au kuolewa kwenye miji au vijiji walikotokea kuna changia Wanandoa wengi kujikuta wana sura zinazofanana kutokana na makabila mengi kuwa na sifa moja inayofanana mfano pua nyembaba, pua kubwa, macho madogo n.k

Sababu nyingine waliyoitoa ya kwanini Wanandoa wengine sio kabila moja lakini bado wanafanana, wanasema kwa kawaida ubongo wa binadamu huwa na hali ya kumuamini mtu ambaye anavitu vinavyoendana na yeye na hali hii hupelekea watu kuoa au kuolewa na watu wanaofana vitu.

Staa wa 50 shades of grey Benedict Cumberbatch na Mke wake

Akielezea sababu ya kwanini wanandoa ambao walikua hawafanani hapo kabla kuanza kufanana baada ya miaka mingi kwenye ndoa, Mwanasaikolojia Robert Zajonc alisema jinsi wanandoa wanavyoishi inapelekea kufanana mfano Mwanaume anaye kasirika sana hutengeza mikunjo kwenye uso wake na Mwanaume wa aina hii humkasirisha mke wake pia ambaye naye atatengeza mikunjo ya uso hivyo kujikuta wamefanana.

Umepata chochote baada ya maelezo hayo? usiache kuniandikia comment yako mtu wa nguvu

VIDEO: Ulipitwa? Flora Mbasha kaolewa tena, mume mpya anaitwa Daud… tazama kila kitu kwenye hii video hapa chini

EXCLUSIVE VIDEO: Mume mpya wa Flora afunguka baada ya ndoa, kila kitu kiko kwenye hii video hapa chini

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

Soma na hizi

Tupia Comments