Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe aliongea na Waandishi wa Habari Dodoma mapema leo May 31, 2017 kuthibitisha taarifa za kifo cha Mwenyekiti wa CHADEMAMkoa wa Kilimanjaro na aliyewahi kuwa Mbunge wa Moshi Mjini Philemon Ndesamburomaarufu kama Ndesapesa.
Kifo cha Mwanasiasa huyo kimeshtua watu wengi hasa wakiwemo wanasiasa ambao wameelezea kusikitishwa na msiba huo huku wakitumia account zao za mitandao ya kijamii kuelezea hisia zao.
Kitila Mkumbo: “Such a loss! Huwezi kuzungumzia maendeleo ya Kilim. na mfumo wa vyama vingi nchini bila kumtaja Mzee Ndesamburo. Apumzike kwa amani!”
Such a loss! Huwezi kuzungumzia maendeleo ya Kilim. na mfumo wa vyama vingi nchini bila kumtaja Mzee Ndesamburo. Apumzike kwa amani!
— Kitila Mkumbo (PhD) (@kitilam) May 31, 2017
Zitto Kabwe aliandika: “#RIPNdesa Mchango wake katika kupigania Demokrasia nchini ni wa kupigiwa mfano. Leo tunafaidi matunda ya Vyama vingi Kwa sababu ya kazi zake…Bungeni alikuwa mstari wa mbele kutaka uhifadhi wa mlima Kilimanjaro kutokana na tishio la theluji kuondoka in our life time.”
#RIPNdesa Mchango wake katika kupigania Demokrasia nchini ni wa kupigiwa mfano. Leo tunafaidi matunda ya Vyama vingi Kwa sababu ya kazi zake
— Zitto MwamiRuyagwa Kabwe (@zittokabwe) May 31, 2017
Professor Jay akaandika kwenye Instagram: “R.i.p Mzee NDESAMBULO. Tumepoteza nguzo muhimu sana. Tanguliza Mzee wetu nasi tunafuatia!!”
VIDEO: Alichoongea Mbowe baada ya taarifa za kifo cha Ndesamburo!!