Ad
Ad

Top Stories

Ndugai afichua kilichoItesa CCM Uchaguzi Mkuu 2020

on

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema kuwa CCM ilipata wakati mgumu kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2021 kutokana na wanawake kutozwa tozo wanapojifungua.

Ndugai ambaye ni mbunge wa Kongwa amesema kuna haja ya kuangalia kwa kuwa wanachozungumza wabunge kina ukweli na walikiona kwenye kampeni hasa mkoani Tabora.

Kauli ya Spika ilifuatiwa na swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalum, Hawa Mwaifunga aliyehoji kama Serikali inajua kuwa katika baadhi ya hospitali wanawatoza Sh50,000 wanaojifungua watoto wa kiume na Sh40,000 wanaojifungua watoto wa kike.

“Naomba sana mlitazame hilo watu wa Serikali maana lilitusumbua sana kwenye kampeni na sasa mkoani Tabora, jambo hilo lazima mlitazame kwa namna yake,” Ndugai.

MREMBO MDOGO MUUZA SAMAKI, NYANYA ANAINGIZA MAMILIONI “NALIMA MPAKA NALALA SHAMBA, NIMEAJIRI”

Soma na hizi

Tupia Comments