Spika Job Ndugai leo Jumatatu May 24, 2021 amewaapisha Wabunge wawili wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wabunge hao ni Kavejuru Felix (Buhigwe) na Dkt. Florence Samizi (Muhambwe).
Wabunge hao wamepatikana kufuatia uchaguzi mdogo uliofangika May 16,2021, uchaguzi mdogo wa Muhambwe, Kigoma ulifanyika baada ya kiti hicho kuwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Atashasta Nditiye.
Kwa upande wa uchaguzi mdogo wa Buhigwe, Kigoma umefanyika baada ya kiti hicho kuwa wazi kufuatia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Dr.Philip Mpango kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania March 30,2021 na hivyo kukoma kuwa Mbunge kwa mujibu wa Ibara ya 71(1)(e) ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.
MDOGO WA JIMMSON ASIMULIA AIBUKA MAPYA MAJAMBAZI WALIVYOMVAMIA KAKA YAKE, “DAMU ILIMUISHIA”