Baada ya jana kutolewa kwa taarifa inayohusu kubainika kwa makontena 256 yenye mchanga wa dhahabu katika Bandari ya Dar es Salaam, leo tarehe 25 March, 2017 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai na wajumbe wa kamati za Bunge za Bajeti na Nishati na Madini wametembelea kwenye Bandari hiyo.
Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai na wajumbe wa Kamati za Bunge za Bajeti na Nishati na Madini wamejionea makontena yenye mchanga wa dhahabu kutoka mgodini yaliyokuwa yamezuiawa kusafirishwa nje ya nchi kwa agizo la Serikali.
Akizungumza baada ya kuona makontena hayo Spika Ndugai amesema…..>>>Kupitia timu tutakayoiunda tunataka kujua nani anasimamia biashara hii kuanzia kwenye chanzo mpaka hapa ‘bandarini’ na huko yanakoenda madini yetu, nani anasimamia maslahi yetu kule, kama ni Ujerumani nani anasimamia, unapelekaje mali yako mahali amabko hakuna hakuna anayekuangaliazia’
VIDEO; Makontena mengine 262 yenye mchanga wa madini yabainika bandari ya DSM, Bonyeza play hapa chini