Ni headlines kutokea mkoani Morogoro ambapo kata ya Kilakala Manispaa ya Morogoro wameingia katika vichwa vya habari baada ya familia ya Mzee Gervas Chondoma Mkoba kuchukua mwili wa mtu mwingine na kuuzika wakidhani kuwa ni ndugu yao ambao mwili wake ulihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya rufaa ya mkoa wa morogoro.
Mwenyekiti wa Mtaa huo Justine Mkoba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, amesema mwili huo uliyedhaniwa kuwa ni Marehemu Gervas Chondoma Mkoba ulizikwa tarehe kumi mwezi huu na kufukuliwa tarehe kumi na moja mwezi huu, huku pande zote mbili za marehemu wakikubaliana kubadilishana miili hiyo ya marehemu ambao wanafanana majina yao ya kwanza .
Ayo TV & Millardayo.com imekusogezea hapa taarifa kamili ushuhudie yale yaliyojiri
KABURI LILILOFUKULIWA NA KUTOLEWA MWILI, SABABU YAELEZWA ‘WALIPOKWENDA MOCHWARI HAWAKUKUTA MWILI”