Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro amepokea taarifa ya Kamati iliyoundwa mwezi Aprili mwaka huu kuchunguza tuhuma za ubadhirifu wa fedha pamoja na masuala ya Rasilimali Watu zinazoikabili Bodi ya Utalii.
Dkt. Ndumbaro akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Allan Kijazi wamepokea taarifa ya kamati hiyo iliyoundwa kuchunguza ubadhirifu huo ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Bw. John Mtega katika makabidhiano yalioyofanyika jijini Dar es Salaam.
Ubadhilifu wa fedha katika bodi hiyo iliyopelekea kusimamishwa kazi Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Devotha Mdachi Aprili 10, 2021 ili kupisha uchunguzi na kupekelea kuundwa kwa Kamati hiyo.