Habari za Mastaa

Mabibi na Mabwana!! ushindi huu ni wa Nedy Music AFRIMA 2018

on

Mwimbaji wa Bongo Fleva Nedy Music ambaye pia yupo chini ya record label ya PKP ameshinda tuzo ya ‘African Fans Favourite” katika tuzo za AFRIMMA zilizofanyika November 24 2018 Ghana.

Nedy Music ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwashukuru wale wote waliompigia kura ikiwa pamoja na wimbo uliomfanya apate tuzo hiyo “One and Only” aliomshirikisha Ruby.

Neddy Music ameandika >>>Asante Mungu🙏Safari hii imekuwa kubwa na yenye matunda sana kwangu . Ninamshukuru Mungu, familia yangu, timu yangu na Mashabiki wangu wote ndani na nje kwa kunisapoti hasa kijana wenu katika kazi yangu ya muziki na Kuhakikisha nasukuma gurudumu la muziki mbele zaidi”

“Bila kusahau Vyombo vyote vya Habari Tanzania na duniani kote, yote ilianza kama ndoto lakini kujiamini kwa kile nilichokua nafanya kwa bidii na kuzingatia kile nilichokua nataka mbeleni ingali bado safar ni ndefu kwangu….sisemi haya kwa kujisifu lakini kuwa mshindi kwenye tuzo kubwa kama hii ambazo zinaunganisha mataifa 52 Ni kubwa sana kwangu na Nchi yangu pia 🇹🇿”

“Mashabiki wangu wote na wapenda burudani ambao hamkuchoka kupiga kura kila sku Asanteni sana sana,🙏🙏Naomba mzidi kunisapot nami nawaahidi kutowaangusha… Kubwa Zangu Shukran kwa My Brother @ommydimpoz Kwa Jinsi ulivyonishika na kunisaidia kusogeza hatua yangu sitaacha kutoa shukran zangu kwako”

“Kila hatua ntayoendelea nayo kwangu🙏 Pia Producer wa Wimbo uliopelekea kuwa kwenye kinyang’anyiro @yogobeats🙏 na msanii nilieshiriki nae fika @iamrubyafrica Bila kumsahau Bwana Director @hanscana_ 🤝 Thanks @afrimawards for this award🙏 “African fan’s favourite “ 🏆

MICHAEL JACKSON WA TANZANIA AKICHEZA “HOLD ME” YA MICHAEL JACKSON, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA

GIGY MONEY: “NILIUZA MWILI WANGU ILI NIMLIPIE MAMA YANGU DENI BENKI” BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments