May 16 2016 Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imewasilisha Bungeni Makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2016/2017 pamoja na kuwasilisha maombi ya fedha zaidi ya Bilioni 864. Hotuba imesomwa na Waziri wake Charles Kitwanga.
Waziri Kitwanga amesema..>>> ‘Wizara yangu imeendelea kupokea na kushughulikia malalamiko ya watumishi ndani ya vyombo Wizara pamoja na wananchi wanaolalamikia utendaji wa vyombo hivyo’
‘Katika kipindi cha Julai 2015 hadi Machi 2016 Wizara kupitia idara ya malalamiko 238 yanayohusu utendaji kazi wa vyombo vya kijeshi ndani ya Wizara kutoka kwa wananchi kupitia njia ya barua, simu, barua pepe, nukushi pamoja na mahojiano’
‘Ili kuiwezesha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kutekeleza majukumu yake katika mwaka wa fedha 2016/2017, naliomba Bunge lipitishe makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ya jumla ya Shilingi 864,106,290,105‘
‘Kati ya fedha hizo shilingi 316,126,377,000 ni za matumizi mengineyo, Shilingi 500,056,492,000 kwa ajili ya mishahara na Shilingi 47,923,421,105 ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo‘
ULIIKOSA HII MBUNGE ALIYETAMANI HATA KULIA DODOMA KISA BUNGE LIVE?
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE