Mix

Hili ndo tamko la Jeshi la Polisi Nchini kuhusu kutekwa kwa Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Temeke

on

DSC_0026Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaama Suleiman Kova ameongea na Waandishi wa Habari na kutoa tamko kama Jeshi la Polisi Nchini kuhusiana na kutekwa kwa Mwnyekiti wa Chadema Wilaya ya Temeke Joseph Yona,hivi ndivyo alivyoanza kuongea na waandishi

DSC_0033‘Katika tukio la kutekwa nyara Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Temeke anayeitwa Joseph Yona ni kwamba tumeamua kufatilia kwa makini matukio kama haya lakini habari kwa ufupi ni kwamba huyo mlalamikaji Joseph Yona alitoa taarifa za kutekwa kwake na baadae kutupwa vichakani kule eneo la Ununio kwa mlinzi ambae alikua kwenye kazi zake za kawaida’

‘kinachoonekana pale kwa uchunguzi wa awali huyu mlalamikaji alikua anapata vinywaji kule Temeke katika Grocery iitwayo Mgumbini walifika watu 6 kwanza walijitambulisha kama maafisa polisi lakini yeye akamtambua mmoja wapo kuwa si Afisa Polisi hiyo ilikua saa 5 usiku’

‘Wakamwambia wanataka kumpeleka kituo cha polisi hawakumueleza kosa walimwambia twende kituo cha polisi sisi ni askari polisi lakini yeye akauliza  kwamba kati ya nyinyi sita mbona huyu mmoja namfahamu kwa sura na jina na mwanachama mwenzangu wa Chadema na  tunafanya nae kazi kila siku mnasemaje nyie wote maafisa wa polisi’

‘Aliposema hivyo wale wakakasirika wakamnyakua haraka wakamuingiza kwenye Gari aina ya Landcruiser wakachukua kitamabaa wakamfunika usoni ili asiendelee kuwaona tena huku wanamhoji katika mahojiano yao ndani ya gari’

‘Kutokana na maelezo ya mlalamikaji walikua wanamhoji kwa nini anaendelea kumuunga mkono au kumshabikia Zitto Kabwe wa Chadema na vile vile walikuwa wanataka wamuonyeshe rafiki yake ambaye nae ni mwanachama wa Chadema kwamba nae apatikane haraka sasa huyo mlalamikaji hakuwapa ushirikiano wa kumuonyesha rafiki yake huyo mwingine  ambae nae ni mwanachama wa Chadema’

‘kwa hiyo walichokifanya sasa wakaanza kumpiga huku wakimuhoji masuala mbalimbali mpaka alipopoteza fahamu na alipigwa zaidi alipohoji mnasema mannanipeleka Central mbona hatufiki Kwa hiyo tukio hili moja kwa moja ni tukio la utekaji nyara ambalo ni kosa kubwa sana katika nchi yoyote ukiachilia mbali Tanzania’

‘Sisi tunasema hivi nimeunda jopo la wapelelezi chini ya Mkuu wa Upelelezi kanda maalum Japhary Mohamed  na assistant commissioner  ambao nimewapa maagizo wafanye  upelelezi wa haraka mno na bahati nzuri mlalamikaji ana ushirikiano mzuri na ana akili zake hao watuhumiwa nimesema wapatikane haraka kwa speed kali kadri inavyowezekana ili hatua kali za kiseria ziweze kuchukuliwa’

‘Kutokana na tukio kama hili natoa onyo kali Mtu yoyote au hasa kikundi kiwe cha dini cha siasa au chochote kile wanapokuwa na mgogoro ni vizuri zaidi wakafata mkondo wa kisheria badala ya kufanya fujo,vurugu,utekaji nyara hii haisadii chochote katika kutatua migogoro’

‘Fuata taratibu za kisheria kuna mahakama kuna mabaraza mengi ya usuluhishi kuna wazee kwenye makundi au vyama kwa sababu tukiacha hivi ikaendelea hivi tutaambukizana katika makund mengine na wale watakaopatikana wajielewe kabisa kwamba watachukuliwa hatua kali sana  za kisheria’

‘Kwa sababu inaonekana ni watu wanaofahamika ushauri wangu wa bure ni bora wajisalimishe kwa sababu hakuna kilichojificha yule mlalamikaji baadhi ya watu anawafahamu kwa hiyo ni bora wajisalimishe wenyewe kwa sababu hata wasipojisalimisha sisi tuna uwezo wa kuwakamata sasa ukikamatwa bila kujisalimisha kuna utofauti  na pale ulipojisalimisha mwenyewe maana angalau utakua umeonyesha ushirikiano’

‘Katika tukio hili hatutofanya ajizi  hakuna atakaesalimika kwa wale watakaokuwa wamehusika  katika tukio hili hatutojali nafasi gani unayo katika jamii,yoyote yule atakae tajwa kwa namna moja au nyingine alishiriki,alichochea au alipanga wote wale watakamatwa watashughulikia ili kuondoa huu mtandao wa utekaji nyara

‘Nchi yetu ni nchi ya amani hatupendi vitu vya utekaji nyara ni tishio kubwa kwa usalama wa wananchi wa kawaida na hatawatu wengine wenye nafasi  tofauti’.

 

 

Tupia Comments