Mix

Alienda Nepal kutoa msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi… kilichomtokea kinasikitisha!

on

Dahlia Yehia alikuwa ni msichana mwenye furaha, amani na moyo wa kuwasaidia watu wenye shida lakini ndoto zake zilifupishwa baada ya safari yake ya kwenda Nepal kwenda vibaya!

Miezi michache iliyopita Dahlia alisafiri kwenda Nepal kwa dhamira ya kwenda kutoa msaada kwa watu walioathirika na tetemeko la ardhi… alipofika huko Dahlia alikuwa anawasiliana na ndugu zake kama kawaida kupita Whatsapp na kuwapa maendeleo ya hali ya Nepal.

CNN3

Dahlia na marafiki zake.

Ghafla mawasiliano yakakata baada ya message yake ya mwisho ya Whatsapp tarehe 6 mwezi August, familia na marafiki wakashikwa na wasiwasi na kuwaza pengine kitu kibaya kimemtokea na ameshindwa kuwasiliana na ndugu zake nyumbani… mwezi ukaisha lakini bado kukawa hakuna mawasiliano yoyote kutoka kwa Dahlia.

Wiki iliyopita familia ya Dahlia ilipokea simu kutoka kwa Ubalozi wa Marekani na ndipo walipo pokea taarifa ya kuhuzunisha sana juu ya ndugu yao… Mkuu wa Polisi wa kituo cha Kaski District Police Hari Bahadur Pal aliwaambia familia ya Dahlia kuwa mwanaume aliekuwa mwenyeji wa Dahlia, Nepal amejisalimisha kwa polisi na kukiri kumpiga dada huyo mpaka kumuua na kuutupa mwili wake mtoni!

CNN4

Dahlia Yehia alikuwa na miaka 25 tu!

Baada ya kujisalimisha kwa Polisi tarehe 4 September, mwanaume huyo mwenye jina Narayan Paudel aliomba kukiri kosa lake na kisha akajaribu kujiua kwa kuruka dirisha la kituoni hapo… Polisi wa Nepal bado wanaendelea kuutafuta mwili wa Dahlia ili uweze kurudishwa Michigan kwa ndugu zake.

Sababu kubwa ya kwanini mwanaume huyo aliamua kuchukua maisha ya Dahlia bado haijajulikana ila kwa sasa mwanaume huyo yupo chini ya ulinzi wa polisi kwa ushirikiano na Ubalozi wa Marekani.

Kwa taarifa zaidi unaweza ukatazama hii video hapa chini.

https://youtu.be/31gRTFDbB3Q

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi>>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata piausisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments