Baraza la mawaziri la Israel lilipaswa kukutana ili kujadili makubaliano na Hamas ambayo yangewafanya kubadilishana mateka na wafungwa – lakini hili sasa limefutwa na waziri mkuu wa nchi hiyo, Benjamin Netanyahu.
Jambo la pili katika ajenda hiyo lingekuwa jinsi Gaza ingeonekana siku moja baada ya vita – jambo ambalo mshirika wa Israel Marekani imekuwa ikihimiza kujadiliwa.
Lakini Bezalel Smotrich, kutoka chama cha muungano cha Bw Netanyahu, inasemekana hakutaka mjadala huo ufanyike na amekataa Mamlaka ya Palestina (PA) kuwa na utawala wowote huko Gaza baada ya vita.
Pia anapinga sana kuhamisha pesa yoyote kwa PA kama Wamarekani wamekuwa wakihimiza.
Kwa hivyo chini ya shinikizo na huku kukiwa na hofu ya kusambaratisha muungano wake na kuweka serikali na nafasi yake kama waziri mkuu hatarini, Bw Netanyahu ameghairi mkutano huo, na kuliachia baraza la mawaziri la usalama zaidi.