Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameomba ‘radhi’ Waisraeli kutokana na vifo vya mateka wakati maandamano yakiendelea
Mgomo wa jumla uliitishwa nchini Israel Jumatatu Septemba 2 ambapo baadae waziri Netanyahu alionekana akizungumza katika Ikulu ya Washington, Jumatano, Julai 24, 2024.
Kauli yake ilikuja wakati kukiwa na maandamano makali ya barabarani kuhusu kushughulikia kwake mazungumzo, maandamamano yaliyoingia usiku wa pili huko Israeli.
Shinikizo linaongezeka kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kutaka kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa huko Gaza.
Uhamasishaji huo uliongezeka nchini Israel, haswa baada ya jeshi kutoa tangazo siku ya Jumapili Septemba 1 la kupatikana kwa miili sita ya mateka wa Israeli kwenye handaki kusini mwa Gaza.
“Maumivu ambayo hugeuka kuwa hasira,” Gazeti la kila siku la Haaretzliliandika kwenye kichwa cha habari siku ya Jumatatu asubuhi.
Makumi ya maelfu ya Waisraeli waliandamana siku ya Jumapili na kudai makubaliano ya kuachiliwa kwa mateka, bila kuchelewa.