Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisimama kizimbani kutoa ushahidi kwa mara ya kwanza Jumanne katika kesi yake ya muda mrefu ya rushwa ili kutoa ushahidi ambao huenda ukamlazimu kucheza kwa wiki kadhaa kati ya mahakama na chumba cha vita.
Netanyahu, 75, ndiye waziri mkuu wa kwanza wa Israel aliyeko madarakani kushtakiwa kwa uhalifu kam huo na ndiye kiongozi aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi nchini, akiwa madarakani takriban mfululizo tangu 2009 kwa mujibu wa reuters.
“Nimekuwa nikingoja kwa miaka nane kwa wakati huu kusema ukweli,” Netanyahu aliwaambia majaji watatu wanaosikiliza kesi hiyo. “Lakini mimi pia ni waziri mkuu “Ninaiongoza Israeli na Taifa la Israeli katika nyanja saba ya vita, Na nadhani haya mawili yanaweza kufanywa kwa usawa.”
Kesi hiyo ilihamishwa kutoka Jerusalem kwa sababu za kiusalama ambazo hazijajulikana na kuitishwa katika mahakama ya chinichini, umbali wa dakika 15 kutoka makao makuu ya ulinzi nchini humo.
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, pia alijibu kuhusu madai kwamba alijipatia shampeni na sigara na kutumia nafasi yake kupata maelfu ya shekeli za faida binafsi.
“Huu ni uongo mtupu. Ninafanya kazi masaa 17, 18 kwa siku. Kila anayenijua anajua hili,” anasema. “Ndivyo ninavyofanya kazi. Ninakula chakula changu kwenye meza yangu ya kazi, sio cordon bleu, sio wahudumu wanaokuja na glavu nyeupe kunihudumia”
Waziri mkuu asema kwamba “nyakati fulani mimi huketi na sigara, na siwezi kuivuta yote mara moja kwa sababu ninaivuta kati ya mikutano.” Anaongeza, “Ninachukia champagne, siwezi kunywa hivyo madai hayo ni upuuzi.”