Waziri mkuu wa Israel amefika katika mahakama ya Tel Aviv kuendelea kutoa ushahidi wake katika kesi yake ya muda mrefu ya rushwa.
Mzee huyo mwenye umri wa miaka 75 amefunguliwa mashtaka katika kesi tatu zinazohusu zawadi kutoka kwa marafiki mamilionea na kwa madai ya kutafuta upendeleo wa udhibiti kwa matajiri wa vyombo vya habari ili kujitangaza vyema.
Anatuhumiwa kwa kupokea maelfu ya dola za Kimarekani, sigara na mvinyo wa bei ghali aina ya ‘champagne’ kutoka kwa bilionea mmoja mtayarishaji wa filamu wa Hollywood kwa makubaliano kwamba Netanyahu angelimsaidia katika mambo ya kibinafsi na ya kibiashara.
Netanyahu, ambaye anakanusha makosa yoyote, amekana hatia