Katika Jiji la New Mexico Marekani, sehemu kubwa sana ya eneo la Jiji hilo ni Jangwa na Milima mikubwa… ni eneo kame kabisa ambalo sio rahisi mtu akavutiwa kuishi.
Wataalam wa Masuala ya Teknolojia wamekuja na hii mpya mtu wangu, hapohapo New Mexico linajengwa Jiji la Kisasa.
Hilo eneo litakuwa na kila kitu kama Jiji ambalo lina makazi ya watu, ikiwemo mitaa ya kisasa na iliyopangika vizuri, nyumba, sehemu za hifadhi, maduka na malls kubwa.
Jiji litaitwa ‘The CITE (Center for Innovation, Testing and Evaluation)’, lakini hakuna mtu hata mmoja ambayo atabahatika kuishi hapo kwa sababu Jiji limeandaliwa kwa matumizi maalum kabisa !!
Kazi ikikamilika mwaka 2018 hili eneo litakuwa na matumizi mengi ikiwemo kufanyika majaribio ya Teknolojia mpya ikiwemo mifumo ya ujenzi wa Barabara, Majengo, Mawasiliano na Ulinzi.
Ukitaka kuthibitisha kwamba Marekani wako fiti na mipango yao, hili Jiji litakuwa na kazi maalum kama ambavyo waliweza kuitenga Hollywood kuwa sehemu ya masuala yote ya burudani ikiwemo kuchezea movies… hiyo inarahisisha sana vitu kufanyika kwa urahisi tofauti na kufanyia sehemu ambayo ina msongamano wa makazi ya watu na shughuli nyingine zinaendelea.
Bajeti ambayo imetengwa ni kama Dola Bilioni moja ambayo inagonga mpaka Trilioni 2.1 kwa hesabu ya pesa ya Tanzania… na unaambiwa kama ingetokea watu wanaruhusiwa kuishi hapo, jumla ya watu 35,000 wangepata makazi.
Unaweza kucheki pia story yote kwenye kipande cha Video.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE