Habari za Mastaa

Diamond kwenye headlines tena na video mpya, sasa hivi ni ft. Khadija Kopa kwenye hii taarabu ‘nasema nawe’

on

d 12Nitampata Wapi‘ ni hit ya mkali anayeiwakilisha vizuri TZ kupitia muziki anaoufanya, Diamond Platnumz.. Jina lake sio geni kwa wapenzi wa muziki Afrika.

Ngoma hiyo aliyoitoa mara ya mwisho bado inafanya vizuri.. Wanigeria wanatoa ngoma mpya kila siku, Diamond  nae anataka kuwa kama wao?

Kupitia ukurasa wake wa Instagram alishare teaser ya video ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘Nasema Nawe‘ ambao audio yake tayari iko mtaani halafu akaandika hivi; “Naombeni Ruksa zenu waungwana nianze Kuzifumua…@

Dakika chache baadae ameiweka video hiyo Youtube, kumaanisha kwamba ndio tayari imetoka yani..

Amefanya video nyingi nje ya TZ ikiwemo South Africa na Nigeria.. safari hii VIDEO kaifanya TZ na Director ni Mbongo Hanscana.. Play hapa mtu wangu…

Unataka Diamond asome maneno yako baada ya kuitazama hii video? niachie comment yako hapa chini

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments