Ad

Top Stories

Nimethibitishiwa kuhusu Dk. Magufuli kufanya uteuzi wa Mwanasheria Mkuu TZ.. (+Audio)

on

Ni saa chache tu zimepita toka Rais wa awamu ya tano, Dk. John Pombe Magufuli aapishwe na kuanza kazi yake kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Makamu wake, Mama Samia Suluhu Hassan… mpya nyingine ni juu ya uteuzi wa Mwanasheria Mkuu anayeanza majukumu yake mapya kwenye Serikali ya tano inayoongozwa na ‘Tingatinga Magufuli

Masaju

Kazi imeanza, Rais Magufuli amemteua George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kesho November 06 2015 ataapishwa Ikulu Dar es Salaam.

Mwanasheria huyo sio mgeni kwenye nafasi hiyo, George Masaju alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliyomaliza muda wake iliyoongozwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ambapo aliishika nafasi hiyo baada ya aliyekuwa anaongoza wakati huo, Jaji Frederick Werema kujiuzulu December 2014 wakati wa sakata la ESCROW.

Niliirekodi taarifa hiyo kwenye Ripoti za habari ya kituo cha TV Channel Ten.. hii hapa kwenye audio.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments