Habari za Mastaa

Unamkumbuka Naj? Kutana na muonekano wake mpya kwenye ‘No Going Home’ – (Video)!

on

Good news kwa watu wangu wa Bongo Flevani, baada ya ukimya wa muda mrefu msanii wa muziki wa Bongo Fleva aliyekuwa Uingereza kwa ajili ya masomo, Naj amerudi kuichukua nafasi yake kwenye kurasa za burudani Tanzania!

NAJ

Najua imepita muda mrefu sana toka tusikie midundo ya Naj kwenye radio na TV, ila kama haijakufikia basi ipokee hii popote pale ulipo… Naj amerudi na fleva, style na mdundo tofauti kwenye muziki wa Bongo Fleva… na muonekano wake mpya na vingine vingi unaweza kuvinasa kwenye official music video ya single yake mpya, ‘No Going Home’.

NAJDAT3

Kwenye kichupa chake kipya, Naj anaongeza fleva ya muziki wake kwa kuonyesha swagger na style fulani ya kurap maneno yanayosema…Like a hipster don wanna lie, niwapo nawe kila time nafurahi, they ask me, me i tell dem i don know why, it’s me and you till I die…

NAJDAT

Mdundo huu umetengenezwa hapa hapa Dar es salaam huku Director wa video mpya ya Naj akiwa Simon Dewey kutokea kampuni ya Epik Music Videos. Kukutana na mdundo mpya wa Naj, bonyeza play hapa chini.

Unaweza pia ukakaa karibu na Naj kupitia page yake ya Instagram @najdattani.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments