Top Stories

Kauli ya leo ya Chadema kuhusu Mwenyekiti wake kutekwa, mpya ya Polisi kuwashika kadhaa ipo pia

on

ununio6Ni headlines ambazo zimemiliki vyombo vya habari toka jana January 7 2014 kuhusu Mwenyekiti huyu wa Chadema wilayani Temeke Dar es salaam Joseph Yona kutekwa, kupigwa na kutupwa saa tisa usiku Ununio wilayani Kinondoni Dar es salaam.

Anasema baada ya kuchukuliwa baa na watu waliokua na gari kama la Polisi na kujitambulisha kwamba ni Polisi, walimwambia wanampeleka Central lakini walipokua njiani wakamziba uso kwa nguo na kuanza kumpiga kabla ya kumtupa.

Mpaka jana jioni wakati inamalizika kesi ya Zitto Kabwe dhidi ya CHADEMA Mahakama kuu kanda ya Dsm, Mh. Tundu Lissu alisema hajui chochote kuhusu kupigwa kwa Mwenyekiti huyu na ndio kwanza alikua anazisikia hizo taarifa wakati anaulizwa jioni hiyo.

Leo Chadema kupitia katibu wa chama hicho Dar es salaam Henry Kilewo kimesema ‘tunalitaka jeshi la polisi kuchunguza hili tukio ili ukweli ujulikane na haki itendeke kwa sheria kuchukua mkondo wake, vilevile jeshi la Polisi linapaswa kuyachukulia kwa uzito mkubwa matukio ya aina hii yanayoanza kuota mzizi kutokana na watu waovu wanaotekeleza na kutokuchukuliwa hatua za kisheria’

ununio7Baada ya hii kauli ya Chadema, Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova anasema ‘mpaka sasa tumeshakamata watu wawili ambao siwezi kuwataja, ni kati ya wale waliosemekana kufanya huu utekaji na bado oparesheni inaendelea’

Tupia Comments