Miji/Nchi

Kama ulishangaa mastaa wa bongo kufanya siasa, kuna Rais ni comedian na kaapishwa Guatemala.. (+Video)

on

Wako mastaa waliojaribu maisha kwenye upande mwingine Tanzania, wako waliotoka kwenye game ya muziki na wengine walitoka kwenye movie… kwa maamuzi ya dhati kabisa wakajitangaza kwamba wanaitaka siasa !!

Wapo waliotoboa, wakafanikiwa kupata nafasi walizogombea kwenye Ubunge na Udiwani lakini wako ambao mambo hayakwenda sawa na wakaahidi kwamba wanaingia mtaani kujipanga rasmi kwa ajili ya jukwaa la kampeni za 2020 Tanzania.

jimmymorales

Rais Jimmy Morales

Kama ambavyo mwigizaji Schwarzenegger aliwahi kuwa Gavana wa Jimbo la California kuanzia mwaka 2003 mpaka 2011… hiyo ni nafasi kubwa sana kwa Marekani, lakini mwingine kutoka kwenye mikono ya sanaa ya uigizaji na vichekesho GuatemalaJimmy Morales ameshinda kiti cha Urais na tayari kaapishwa.

Rais huyo mpya hana uzoefu na masuala ya siasa ila ahadi yake ya kwanza ni kupambana na rushwa…

Hii hapa video ya Jimmy Morales akiwa anaapishwa nchini kwao Guatemala.

Kipande kingine hiki hapa cha stori siku alivyochaguliwa pamoja na sehemu ya comedy zake.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments