Magazeti

Mapya ya Mtanzania anayehusishwa na Ugaidi Kenya,GWAJIMA kuhojiwa leo na Vigogo wa RUBADA kusimamishwa..#MAGAZETINI APRIL9

on

WEL

MTANZANIA

Wazazi wa Mtanzania Rashid Charles Mberesero (21), anayetuhumiwa kuwa mmoja wa wanamgambo wa Al-Shabaab ambao walifanya mauaji katika Chuo Kikuu cha Garissa nchini Kenya na kuua wanafunzi 148, wamefunguka na kueleza siri ya mtoto wao huyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, walisema wakati kijana huyo akihusishwa na tukio hilo lililotokea Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo, walikuwa wakijua mtoto wao yupo shuleni mkoani Dodoma.

Baba mzazi wa mtoto huyo, Charles Mberesero, alisema mwanawe huyo ni mwanafunzi wa kidato cha tano katika Shule ya Sekondari Bihawana iliyopo mjini Dodoma.

Alisema kwa muda mrefu mtoto wake alikuwa akilelewa na mama yake mzazi huko Gonja, Same mkoani Kilimanjaro, lakini kwa muda mfupi alioishi naye hakuwahi kufikiri kwamba angeweza kujihusisha na tukio kama hilo.

Rashid alizaliwa mwaka 1994 huko Gonja Same, shule ya msingi aliyosoma siikumbuki, lakini sekondari najua kidato cha kwanza hadi cha nne alisoma katika Shule ya Gonja,”Mberesero.

Akimwelezea tabia yake, alisema Rashid ni kijana mtaratibu na mvumilivu sana.

“Alipokuwa akisoma O’ level nilikuwa nawasiliana naye sana, lakini kama mwaka mmoja na nusu uliopita tulikuwa hatuna mawasiliano ya karibu.

“Sasa hivi alikuwa anasoma PCB kwenye Sekondari ya Bihawana Dodoma. Kwenye matokeo ya kidato cha nne alipata daraja la pili na michepuo yote ya masomo ya Sayansi ilikubali, lakini akaamua kusoma PCB,”.

“Juzi baada ya kutokea hayo yaliyotokea huko Kenya niliongea na mama yake, akaniambia mtoto alikuwa likizo ya kama wiki mbili na Machi 21, mwaka huu aliaga nyumbani kwamba anarudi shuleni Dodoma.

“Na unajua mambo ya huko kijijini baada ya mtoto kusema anasafiri kwenda Dodoma shuleni hakuna mtu aliyefuatilia hadi baadaye tulipokuja kusikia hayo ya Kenya.”

Alisema kutokana na alivyoshtushwa na tukio hilo, tangu alivyopata taarifa zake siku ya Jumapili, alipata presha na jana ndipo aliweza kupata ahuweni na kutoka nyumbani.

Baba huyo alisema uhusiano wake na mtoto wake haukuwa mzuri sana kwa sababu alimtaka abadilishe dini yake akakataa.

Nilikuwa namshawishi afuate dini yangu, mimi ni Mkatoliki kwa hiyo kuna wakati alikuja kwangu akakaa kama mwezi mmoja nikawa naenda naye kanisani, nikawa namshawishi abatizwe.

“Alikataa akasema anafuata dini ya mama yake… baada ya kuzaliwa sikumfuatilia sana kwa sababu mama yake aliolewa na mtu mwingine, sasa pale mimi kuzungumza naye kila saa isingewezekana,” .

Mberesero alisema kwa muda aliomjua mtoto wake huyo, anafahamu kwamba si mtu wa kutoka sana nyumbani kwa hiyo anashindwa kujua ni wapi alipojifunzia mambo ya kigaidi.

Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili, mama mzazi wa Rashid, Fatma Ally, alisema mwaka jana mtoto wake huyo alifaulu mtihani wa kidato cha nne na kupangiwa kujiunga na kidato cha tano katika Shule ya Sekondari Kingwe iliyopo mkoani Dodoma.

Alisema alivyofika kwenye shule hiyo alibaini haikuwa na mchepuo wa Sayansi aliokuwa akisoma, hivyo akaomba kuhama na ndipo alipopata nafasi Shule ya Sekondari Bihawana.

“Hakusubiri likizo iishe, akasema kwa sababu sisi ni Waislamu haisubiri Pasaka, nikamwandalia vitu vyake akasema anaenda shuleni,” alisema.

“Hata akiwa nyumbani akitoka sana anaenda msikitini, sijui huo ushawishi kaupata msikitini ama huko shuleni,” alisema
Alisema siku mwanaye huyo anaenda shule, alimpa Sh 90,000 kwa ajili ya nauli na matumizi mengine.

“Hata akiwa shuleni akiniambia ana shida huwa namtumia fedha yoyote niliyonayo, naweza kumtumia Sh 5,000, 10,000 ama 20,000,” alisema.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Bihawana, Mbilinyi Joseph, alithibitisha kwamba Rashid Charles Mberesero ni mwanafunzi wa shule hiyo na tangu mwanafunzi huyo alipoondoka wakati wa likizo Novemba 25, mwaka jana hadi sasa hajarejea shuleni.

MTANZANIA

Serikali  imewasimamisha kazi vigogo watatu wa Mamlaka ya Ustawishaji Bonde la Mto Rufiji (Rubada) kwa muda usiofahamika.
Vigogo hao wamesimamishwa kazi baada ya kutuhumiwa kwa ubadhilifu wa zaidi ya Sh bilioni 2.3.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, aliwataja vigogo hao ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Aloyce Masanja,

Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Tabu Ndatulu na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala,Filozi Mayayi alisema ubadhilifu huo umebainika baada ya tume iliyoundwa na wizara kwa kushirikiana na Hazina kufanya uchunguzi wa kina.

Wasira alisema viongozi hao wamekuwa wakijihusisha na masuala mbalimbali ya kiuongozi, jambo ambalo kamwe Serikali haiwezi kulivumilia.

Alisema amechukua uamuzi huo wa kinidhamu kwa kutumia mamlaka yake ya waziri mwenye dhamana.
Wasira alisema makosa mengine ya kijinai ameiachia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi.

Alisema vigogo hao walikuwa wakiwatoza fedha watu ambao walikuwa wanataka kuwekeza kwenye kilimo.

“Kibaya, hawa viongozi walikuwa wakiwatapeli wawekezaji kwenye sekta ya kilimo kwa kuwatoza fedha bila kuwaonyesha maeneo ya kulima jambo ambalo lilizua malalamiko makubwa,”Wasira.

Alisema zaidi ya Sh bilioni 2.7 zilipokewa na maofisa hao kutoka kwa wawekezaji, lakini fedha zilizoonekana kwenye akaunti ni Sh milioni 714.6 wakati Sh bilioni 2.3 hazijulikani zilipo.

Wasira alisema tayari ameiandikia Bodi ya Wakurugenzi ya Rubada ianzishe mchakato wa kujaza nafasi hizo haraka iwezekanavyo ili kazi ziweze kuendelea kama kawaida.

“Maofisa hawa wakuu walikuwa wakijilipa masurufu na baadhi ya fedha zimegundulika kuwekwa kwenye akaunti zao binafsi badala ya ile ya Rubada.

“Fedha za wafanyakazi zaidi ya Sh milioni 58 walizokuwa wakikatwa kwa ajili ya kupelekwa katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ziliishia mifukoni mwao, taratibu za utoaji tenda zilikiukwa, wamefanya watakavyo,” Wasira.

Alisema mfumo mzima wa utendaji wa mamlaka hiyo ulikuwa dhaifu na hakukuwapo na mgawanyo wa kazi, huku maofisa hao wakiidhinisha malipo na kutembea na fedha mifukoni.

Wasira alisema kazi hiyo ilipaswa kufanywa na mhasibu kama utaratibu wa Serikali unavyotaka.

Rais huyo wa awamu ya tatu aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati wa mahojiano aliyoyafanya na vyombo vya habari kwenye Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC), baada ya kutoa mhadhara kwa wanafunzi wa chuo hicho.

Mkapa alitoa mhadhara kuhusiana na tathmini ya kiuchumi kuelekea vita ya tatu ya dunia.

Mkapa alisema kwa hali ilivyo sasa ni sababu za kiuchumi ndizo zinazoleta vita, kutokana na uongozi mbaya, njaa na kiu ya baadhi ya nchi kutaka maliasili za mataifa mengine.

“Hatutarajii kuwa na vita kama ile ya pili ya dunia, kwa sababu Dunia sasa inamiliki silaha kali kama za nyuklia, zinazoweza kuangamiza maisha kwa wingi, na ndiyo maana unaona mazungumzo kupunguza silaha za nyuklia kama yale ya Iran,” .

Alisema ili kuzuia vita kutokea ndani ya nchi, ama kati ya nchi mbili, ukanda, bara na hata dunia, kuna umuhimu wa serikali zilizoko madarakani na hasa barani Afrika kuwekeza kwenye uongozi bora na kuwashirikisha wananchi katika maamuzi ya kidemokrasia, yanayohusu maisha na rasilimali za nchi zao.

“Ni vizuri kuwa na sera zinazojenga, zisizogawa wananchi katika misingi ya udini na ukabila, kuhakikisha mikataba inayoingiwa juu ya rasilimali za nchi inawanufaisha wananchi na si wageni peke yao, na kama kuna unahitaji wa kuirekebisha, ni bora hilo likafanyika,” .

Alisema mikataba kama ule wa EPA, si ya kuiruhusu kwani mwisho wa siku itaua juhudi za nchi maskini kuendelea, kwa sababu zinalenga kuifanya Afrika kuwa soko la bidhaa za Ulaya.

“Mazungumzo juu ya EPA kwa nchi nyingi zilizo kwenye eneo la Sahara ni kama yamemalizika, kinachosubiriwa sana sana na kuridhiwa na mabunge, lakini mkataba huu kimsingi haufai kwa nchi zetu za Afrika,” alitahadharisha Mkapa.

Mkapa alisema: “Iwapo EPA itaridhiwa na mataifa yetu, itakuwa ni chanzo cha kudhoofisha kilimo chetu, viwanda vyetu, malighafi  hazitasindikwa na maduka yetu yatajaa bidhaa za Ulaya na mwisho wa siku ajira itakosekana.”

Akizungumzia suala la muundo wa sasa wa UNSC, Mkapa alisema: “Kuna umuhimu wa kuifumua taasisi hiyo kwa sababu dunia sasa imebadilika, tofauti na ilivyokuwa wakati inaundwa,”.

Alisema tasisi hiyo inastahili kufumuliwa na kuundwa upya kwa sababu hivi sasa kuna mataifa ambayo yameendelea sana kiuchumi na kiuwezo katika dhana za kivita na hivyo kustahili kuwamo ndani yake.

Alisema mataifa hayo yanastahili kuwamo ndani ya taasisi hiyo kwa sababu ya ushawishi na nafasi yaliyonayo sasa, inayoyafanya yawe na mchango kwenye maamuzi ya taasisi hiyo.

NIPASHE

Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, amezipa angalizo nchi za Kiafrika kukuza uongozi bora na kuachana na mikataba mibovu isiyojali ustawi wa wananchi kwa kuwa inaweza kuzipeleka katika vita.

Miongoni mwa mikataba ambayo amesema kuwa ni mibovu na isiyofaa, hivyo iepukwe ni wa Kiuchumi baina ya Mataifa ya Afrika, Caribbean na Pacific (EPA), ili kuepusha vita, ambayo kwa sasa itakuwa ni ya kiuchumi.

Aidha, ametaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) lifumuliwe ili kuongeza nchi nyingine ambazo zinastahili kuingia kwa sasa.

Rais huyo wa awamu ya tatu aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati wa mahojiano aliyoyafanya na vyombo vya habari kwenye Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC), baada ya kutoa mhadhara kwa wanafunzi wa chuo hicho.

Mkapa alitoa mhadhara kuhusiana na tathmini ya kiuchumi kuelekea vita ya tatu ya dunia.

Mkapa alisema kwa hali ilivyo sasa ni sababu za kiuchumi ndizo zinazoleta vita, kutokana na uongozi mbaya, njaa na kiu ya baadhi ya nchi kutaka maliasili za mataifa mengine.

“Hatutarajii kuwa na vita kama ile ya pili ya dunia, kwa sababu Dunia sasa inamiliki silaha kali kama za nyuklia, zinazoweza kuangamiza maisha kwa wingi, na ndiyo maana unaona mazungumzo kupunguza silaha za nyuklia kama yale ya Iran,” alisema.

Alisema ili kuzuia vita kutokea ndani ya nchi, ama kati ya nchi mbili, ukanda, bara na hata dunia, kuna umuhimu wa serikali zilizoko madarakani na hasa barani Afrika kuwekeza kwenye uongozi bora na kuwashirikisha wananchi katika maamuzi ya kidemokrasia, yanayohusu maisha na rasilimali za nchi zao.

“Ni vizuri kuwa na sera zinazojenga, zisizogawa wananchi katika misingi ya udini na ukabila, kuhakikisha mikataba inayoingiwa juu ya rasilimali za nchi inawanufaisha wananchi na si wageni peke yao, na kama kuna unahitaji wa kuirekebisha, ni bora hilo likafanyika,” alisema.

Alisema mikataba kama ule wa EPA, si ya kuiruhusu kwani mwisho wa siku itaua juhudi za nchi maskini kuendelea, kwa sababu zinalenga kuifanya Afrika kuwa soko la bidhaa za Ulaya.

“Mazungumzo juu ya EPA kwa nchi nyingi zilizo kwenye eneo la Sahara ni kama yamemalizika, kinachosubiriwa sana sana na kuridhiwa na mabunge, lakini mkataba huu kimsingi haufai kwa nchi zetu za Afrika,” alitahadharisha Mkapa.

Mkapa alisema: “Iwapo EPA itaridhiwa na mataifa yetu, itakuwa ni chanzo cha kudhoofisha kilimo chetu, viwanda vyetu, malighafi  hazitasindikwa na maduka yetu yatajaa bidhaa za Ulaya na mwisho wa siku ajira itakosekana.”

Akizungumzia suala la muundo wa sasa wa UNSC, Mkapa alisema: “Kuna umuhimu wa kuifumua taasisi hiyo kwa sababu dunia sasa imebadilika, tofauti na ilivyokuwa wakati inaundwa,”.

Alisema tasisi hiyo inastahili kufumuliwa na kuundwa upya kwa sababu hivi sasa kuna mataifa ambayo yameendelea sana kiuchumi na kiuwezo katika dhana za kivita na hivyo kustahili kuwamo ndani yake.

Alisema mataifa hayo yanastahili kuwamo ndani ya taasisi hiyo kwa sababu ya ushawishi na nafasi yaliyonayo sasa, inayoyafanya yawe na mchango kwenye maamuzi ya taasisi hiyo.

NIPASHE

Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima, anatarajiwa kuhojiwa leo na Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam katika Kituo cha Polisi cha Kati huku wasaidizi wake wakisema afya imeimarika na yupo tayari kwa mahojiano hayo.

Mwanasheria wa Askofu Gwajima, Paul Mallya, alisema jana kuwa mteja wake afya yake imeimarika na yupo tayari kwa mahojiano ya mwisho leo.

Mteja wangu anaeandelea vizuri, kesho (leo) saa mbili asubuhi atahojiwa kama maelekezo ya mwisho ya Jeshi la Polisi yalivyomtaka aende kuhojiwa,” Mallya.

Hata hivyo, Mallya alisema hafahamu kuwa Askofu Gwajima ataongozana na msafara wa watu wangapi huku akisistiza kuwa anachofahamu ni kuwa mteja wake atafika kituo cha polisi cha kati kwa ajili ya mahojiano.

Naye mmoja wa wasaidizi wa karibu wa Askofu ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alilieleza jana  kuwa afya ya kiongozi huyo wa kiroho imeimarika na atakwenda katika mahojiano kama ilivyopangwa, lakini alisema hafahamu ni msafara wa watu wangapi utakaomsikdikiza.

Jitihada za kumtafuta kupitia simu yake ya mkononi Kamanda wa Polisi wa kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, kuzungumzia jinsi polisi walivyojipanga kiulinzi endapo Askofu Gwajima atakwenda kituoni hapo na msafara wa waamini wake, simu yake haikupokelewa.

Aprili 2, mwaka huu Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lilishindwa kumhoji Askofu Gwajima kutokana na kutoridhika na mwenendo wa afya yake, hali iliyomlazimu kuagizwa kurudi tena leo kwa ajili ya mahojiano hayo.

Wakili Mallya, alisema Askofu Gwajima atakwenda Polisi tena kuhojiwa kutokana na mtu aliyetambulika kwa jina la Abubakar Yusufu, mkazi wa Kiluvya, wilaya ya Kisarawe, mkoa wa Pwani,  kufungua kesi ya jinai polisi akilalamika kukwazwa na lugha iliyotumiwa na askofu huyo dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Alisema Yusufu alifungua mashtaka hayo kutokana na picha ya video aliyoiona kwenye mitandao ya kijamii inayomuonyesha Askofu Gwajima akitumia lugha ya matusi kumkashifu Askofu Pengo ambayo  kisheria ni kosa.

Machi 26, mwaka huu, Jeshi la Polisi Kanda hiyo lilimwamuru Askofu Gwajima kujisalimilisha polisi kwa tuhuma za kumkashifu Kardinali Pengo.

Machi 27, Askofu Gwajima alijisalimisha kituo hicho, lakini wakati akihojiwa alizimia akiwa chumba cha mahojiano kisha kukimbizwa katika Hospitali ya TMJ kwa matibabu.

Jumanne ya wiki iliyopita aliondolewa TMJ na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Oyesterbay na kuachiwa bila masharti, lakini alielekezwa kuripoti Alhamisi iliyopitwa katika Kituo cha Polisi Kati.

NIPASHE

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Morogoro, kimetangaza kufanya   maandamano makubwa kwenda kwa uongozi wa Manispaa ya Morogoro, kushinikiza kutekelezwa kauli ya Mbunge wa Jimbo la Morogoro, Abdulaziz Abood (CCM) ya kutaka kutolewa taarifa ya matumizi ya Sh. milioni 720 za mradi mkubwa wa ujenzi wa stendi ya mabasi  yaendayo mikoani eneo la Msamvu.

Pamoja na fedha hizo, pia Chadema inataka maelezo mengine kutoka kwa Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro akiwamo Meya na Mkurugenzi kuhusu fedha za miradi ya  ujenzi  wa soko kuu la Morogoro .

Hatua ya Chadema kuamua kufanya maandamano hayo imekuja siku chache baada ya  Abood kufanya ziara ya kukagua mradi huo na kunyimwa taarifa za matumizi ya fedha ungozi wa manispaa, hivyo kulazimika  kuahirisha ziara hiyo, huku akitoa  siku 14 taarifa hiyo itolewe vinginevyo suala hilo atalifikisha kwa Rais Jakaya Kikwete.

Hata hivyo, uongozi wa Manispaa ya Morogoro kupitia Meya wake, Amir Nondo ukizungumzia suala hilo kwa waandishi wa habari, ulieleza kuwa ujenzi wa mradi unafanywa kwa ubia na Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF) ambao ndiyo wanawajibika na fedha hizo Sh. milioni 720  walizitoa kwa ajili ya fidia ya kumlipa mtu aliyekuwa ndani ya eneo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa jana, Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Morogoro, alisema wanakusudia kufanya maandamano hayo Aprili 14 mwaka huu kwenda ofisi hiyo ya mkurugenzi wa manispaa na meya kutaka matumizi ya fedha za mradi huo wa stendi yawekwe wazi.

Alisema katika mradi huo wa ujenzi wa stendi ya kisasa kuna harufu ya ufisadi unaofanywa na baadhi ya viongozi wa manispaa ndiyo maana wanakataa kutoa taarifa zake kwa mbunge.

Yule ni mbunge anapaswa kujua maendeleo ya ujenzi sasa tunashangaa kwanini wanamnyima taarifa za mradi ambao ni sehemu ya fedha za serikali, kama hakuna ufisadi wanaficha nini?. Sasa sisi tutafanya mandamano ya kumuunga mkono Abood ili wananchi wapewe taarifa za mradi huo na maendeleo yake,” .

Mwenyekiti wa Chadema  alilitaadhalisha Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro kuwa lisithubutu kuyazuia maandamano hayo ya amani, kwani hawatakubali kuzuiliwa kwa kuwa hizo ni fedha za wananchi ambao wengi wao wanashindwa kupata huduma nyingine kama za afya kutokana na mradi huo.

Mradi wa stendi ya kisasa ya mabasi yaendayo mikoani ya Msamvu unatalajiwa kutumia Sh. bilioni 10 katika awamu ya kwanza.

MWANANCHI

Kiongozi wa Chama cha ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe amesema zaidi ya wabunge 50 wa vyama mbalimbali vya siasa nchini watajiunga na chama hicho kipya na kugombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Zitto ambaye alijivua ubunge wa Kigoma Kaskazini baada ya kufukuzwa uanachama wa Chadema, amebainisha kuwa wabunge hao, wakiwamo wa CCM na Chadema, ni miongoni mwa watu wanaokichangia fedha chama hicho kilichopata usajili wa kudumu Mei, mwaka jana na kuzinduliwa mwezi uliopita.

Pia, amewatangazia vita wabunge wa majimbo manane ya Mkoa wa Kigoma, akijigamba kuwa ili waweze kuibuka na ushindi katika uchaguzi huo ni lazima wakubali kujiunga na ACT kwa kuwa chama hicho kimejipanga kuyabeba majimbo yote.

Akizungumza na waandishi wa Mwananchi katika ofisi za gazeti hili, Dar es Salaam jana, Zitto alisema ACT ni chama kilichojipanga na ndiyo maana haikuwa ajabu katika mkutano wake mkuu wa hivi karibuni kuhudhuriwa na wanachama zaidi ya 400 na kufanya uzinduzi wa aina yake, huku akisisitiza kuwa chama hicho kinaungwa mkono na watu wengi.

Tuna wagombea ubunge wengi wakiwamo wabunge wa sasa ambao katika Uchaguzi Mkuu Oktoba hawatagombea kupitia vyama vyao vya sasa. Wapo ambao hawatakwenda hata katika kura za maoni za vyama vyao na wameshafanya uamuzi,Zitto

Huku akizungumza kwa kujiamini, Zitto alisema wabunge hao ndiyo sababu ya chama hicho kuwa na uwezo wa kujiendesha na kufafanua kuwa ACT kinawakaribisha wabunge na makada wote kutoka vyama vya Chadema na CCM.

Wale ambao wanabanwa CCM na kukosa uhuru wa kuhoji jambo lolote hiki (ACT) ndicho chama chao. Wale ambao wanaamini kuwa aina za siasa tulizotaka kuzifanya ndani ya Chadema tukashindwa kuzifanya na wanadhani ni siasa muhimu zinazotakiwa, wapo na sisi,” .

 “Nahitaji majimbo yote ya Kigoma kuchukuliwa na ACT bila kukosa hata moja na hili hata Serukamba (Mbunge wa Kigoma Mjini-CCM) analijua. Mwanasiasa anayetaka kuwa mbunge Kigoma lazima aje ACT,” alisema Zitto ambaye pia alirejea kauli yake kuwa atagombea ubunge katika jimbo jingine lakini siyo Kigoma Kaskazini.

Kauli hiyo ya Zitto inawagusa wabunge wa sasa wa majimbo ya Kigoma ambao ni; Felix Mkosamali (Muhambwe), Moses Machali (Kasulu Mjini), Agripina Buyogela (Kasulu Vijijini) na David Kafulila (Kigoma Kusini), wote wa NCCR-Mageuzi na Peter Serukamba (Kigoma Mjini, Christopher Chiza (Buyungu) na Albert Obama (Manyovu) wa CCM.

MWANANCHI

Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa amesema anashindwa kujitokeza kuzungumzia au kufanya mambo yanayohusiana na urais kwa kuwa Kamati ya Maadili ya CCM inamfuatilia kwa karibu.

Alisema hayo jana alipoulizwa kuhusu kauli ya Rais Jakaya Kikwete wiki iliyopita akiwa Marekani ambako alielezea mafanikio na changamoto alizokumbana nazo wakati wa uongozi wake wa miaka 10.

Kikwete alisema: “Wakati unaingia Ikulu unakuwa na shauku kubwa pamoja na furaha ya ushindi, lakini hakika urais ni kadhia kubwa. Ukipata fursa ya kuwa rais kwa awamu mbili kama mimi nadhani zinatosha kabisa. Nimefanya mengi kwa nchi yangu atakayekuja ataendeleza nilipoishia.”

Kauli ya Lowassa inakuja ikiwa ni siku chache baada ya makada wengine wanaotajwa kuwania urais kupitia CCM kueleza maoni yao juu ya kauli hiyo ya Rais.

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba ameshalieleza gazeti hili kuwa kauli hiyo inampa hamasa kwa nia yake ya kutaka kuwania urais na kwamba alitangaza nia hiyo huku akifahamu kwa asilimia 100 uzito wa jambo hilo akisema kufahamu changamoto hizo ndiyo moja ya vitu vilivyomsukuma kuchukua uamuzi huo.

Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye alisema: “Kama mtu ameamua kuwania nafasi hiyo ina maana anafahamu anachokitaka. Tunajua ziko changamoto na namna ya kukabiliana nazo, kwa hiyo hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi.”

Mbunge wa Nzega, Dk Hamis Kigwangalla alisema: “Kauli kama hiyo haiwezi kumvunja mtu moyo, ari itabaki palepale tu kwa aliyetangaza nia. Aliyetangaza nia anataka kutoa utumishi wake kwa nchi yake kama mimi.”

Lowassa hajatangaza wazi nia hiyo zaidi ya kusema ameshawishika kuwania urais baada ya hivi karibuni, makundi mbalimbali kufika nyumbani kwake mjini Dodoma kumshawishi achukue fomu kuwania nafasi hiyo.

Miongoni mwa makundi yaliyojitokeza na kumshawishi pamoja na kumchangia fedha za kuchukua fomu ya kugombea urais ndani ya CCM ni pamoja na masheikh kutoka wilayani Bagamoyo, wachungaji wa makanisa ya Kipentekoste, wanafunzi wa vyuo vikuu pamoja na madereva bodaboda.

Akizungumza jana wakati wa kuaga mwili wa Mkurugenzi wa zamani wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk Mohamed Mhita nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini Dar es Salaam, Lowassa alisema: “Muda mwafaka ukifika nitatangaza nia na kuweka mikakati yangu wazi ili wananchi waijue.

Kwa sasa siwezi kusema chochote kwa sababu ninatazamwa sana na chama. Ninachoweza kusema, siku nitakayotangaza nia, nitaeleza ni nini nitafanya kukabiliana na changamoto zote zilizopo Ikulu.

MWANANCHI

Upungufu  wa chakula kwa baadhi ya mikoa nchini umeendelea kusababisha ongezeko la mfumuko wa bei wa Taifa kutoka asilimia 4.2 hadi asilimia 4.2 ndani ya mwezi mmoja.

Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ephraimu Kwesigabo, aliwaambia waandishi wa habari leo kuwa, kutokana na upungufu huo bei za bidhaa za vyakula zimeongezeka.

Mfumuko wa bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapimwa kwa kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi,Kwesigabo.

Aliongeza: “Hivyo kutokana na ongezeko la bei za bidhaa hizo pamoja na huduma zote kwa kaya zimesababisha mfumuko wa bei wa taifa,” Kwesigabo.

Aliendelea kueleza kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa hizo zimesababisha mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi iliyopita kuongezeka hadi ukufikia asilimia 4.3 kutoka asilimia 4.2 ya mwezi Februari mwaka huu.

Kwesigabo alisema, ongezeko la mfumuko wa bei kwa mwezi Machi umesababishwa hasa na kuongezeka bei za bidhaa za vyakula kwa kipindi kilichoishia Machi mwaka huu tofauti na ilivyokuwa kwa Machi mwaka jana.

Alizitaja bidhaa hizo kuwa ni pamoja na mchele, unga wa muhogo, nyama, samaki, maharage, choroko na sukari.

Alisema kutokana na hali hiyo wananchi wataendelea kushuhudia bei za vyakula zikiendelea kupanda na kwamba bei waliyokuwa wakinunua bidhaa za vyakula hapo awali itabadilika.

Akizungumzia thamani ya shilingi ya Tanzania kwa mwezi uliopita ikilinganishwa na mwezi Septemba, 2010 alisema, uwezo wa Sh 100 katika kununua bidhaa na huduma umefikia Sh 64 na senti 15 mwezi Machi mwaka huu kutoka Septemba, 2010.

…ikilinganishwa na Sh 64 na senti 59 ilivyokuwa Februari mwaka huu,Kwesigabo.

 HABARILEO

Mzee mwenye umri wa miaka 68, Celestine Mushi, mkazi wa kata ya Motamburu wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, ameuawa na wananchi wanaotajwa kukasirishwa na kitendo chake cha kupeleka waganga wa jadi kijijini kwa lengo la kuifanyia zindiko nyumba yake.

 Mushi anadaiwa kuwatoa waganga hao wawili jijini Dar es Salaam na kuwapeleka Rombo kwa kazi hiyo maalumu.

Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Godfrey Kamwela aliyesema mauaji hayo yalitokea juzi saa 2.30 usiku nyumbani kwa Mushi katika kitongoji cha Mbomai Juu, wakati waganga hao wakiendelea na zindiko lao.

Kamwela aliwataja wanaodhaniwa ni waganga wa jadi kuwa ni Ashraf Mjengwa (22) na Peter Mmaka (25), wote wakazi wa Magomeni, Dar es Salaam.

Alisema waganga hao walifika nyumbani kwa Mushi juzi saa 10 jioni, na ilipofika saa 11 walianza shughuli ya zindiko na walipomaliza, Mushi alitaka kuwapeleka katika nyumba ya mkwe wake aitwaye Priscila Hilment, ili nayo ifanyiwe zindiko.

Kamwela alisema kitendo hicho kilikataliwa na mama mkwe, ambaye alipiga kelele kuomba msaada kwa wananchi ili wawaondoe waganga hao, ambapo wananchi walifika na kuwashambulia waganga hao.

Alisema kutokana na tafrani hiyo, raia mmoja alitoa taarifa katika kituo cha polisi, ambapo polisi walifika eneo la tukio na kufanikiwa kumwokoa mganga mmoja, Mjengwa, ambapo mwenzake alikimbia na kutokomea kusikojulikana.

Kamwela alisema ilipofika saa 2 usiku, kundi la wananchi wasiojulikana idadi yake walirudi nyumbani kwa mzee huyo na kuanza kumpiga kwa fimbo kichwani na sehemu mbalimbali za mwili wake, na kisha kuondoka na kumwacha akivuja damu nyingi.

Alisema kutokana na damu kuendelea kuvuja, mtoto wa mzee huyo alimchukua baba yake na kumpeleka katika kituo cha afya cha Tarakea, ambapo alifariki dunia kabla ya kupatiwa matibabu na Jeshi la Polisi limeanza msako wa kuwatafuta wahusika.

HABARILEO

Wanawake wenye umri mkubwa wametakiwa kuacha kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na vijana wenye umri mdogo, kwani jambo hilo linawapunguzia heshima katika jamii.

Ushauri huo ulitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Halima Kihemba wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Afya Duniani yaliyofanyika eneo la Kituo cha Afya Mlandizi, wilayani Kibaha mkoani Pwani.

Kihemba, ambaye kitaaluma ni mwanahabari, alisema kuna ripoti za kipolisi mkoani Pwani zinazoeleza kuna kinamama ambao tayari wamevuka umri wa miaka 60 wana uhusiano wa kingono na vijana wenye umri mdogo, jambo linalowapunguzia heshima katika jamii.

“Kuna taarifa kuwa miongoni mwenu kuna kina mama wana tabia mbaya ya kuwa na wapenzi ambao ni vijana wadogo sana kiumri. Kweli si kweli? Aliuliza mkuu huyo wa wilaya na wazee hao ambao kwa idadi walikaribia 300, wakaitikia ‘Kweliiiii’.

Akizungumzia ukubwa wa tatizo hilo mkoani humo ambapo alisema “Halijawa tatizo kubwa sana, lakini kuna wachache walio na tabia hizo mbaya, ndio maana tunaanza kulidhibiti ili lisisambae kwa kasi maeneo mengine.” Alisema tatizo hilo kwa ukubwa lipo miongoni mwa wanaume ambao wamekuwa wakijihusisha na ndoa za utotoni kwa muda mrefu, huku likilazimisha wanafunzi wa kike kukatisha masomo yao kuolewa.

 Uchunguzi uliofanywa miongoni mwa wazee ambao walikuwa wanapata huduma ya bure ya kupima afya zao kwa msaada wa shirika lisilo la kiserikali la The Good Samaritan Social Services umethibitisha ubakaji na ndoa za utotoni ni matatizo makubwa maeneo ya Mlandizi na viunga vyake.

Mkurugenzi wa Shirika hilo, Elisha Mwamkinga alisema shirika lake linajitahidi kuwaelimisha wazee kuishi kwa heshima katika jamii na kuepuka mambo ya aibu miongoni mwao.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments